Kuna misimu mikuu miwili, yaani msimu wa mvua na msimu wa kiangazi. Kila mmoja wao una masuala yanayohusiana na ufugaji wa mbuzi.
Hata hivyo, ni bora kuhesabu vizuri ili kuhakikisha kwamba mbuzi wanazaa wakati wa kiangazi kwa sababu katika msimu huo, kunakuwa na maambukizi machache na vile vile ni rahisi kusimamia wanambuzi. Clostridia ndio maambukizi makubwa yanayoathiri wanambuzi na maambukizi haya machache wakati wa kiangazi, lakini huwa mengi sana wakati wa mvua.
Shughuli za usimamizi katika msimu wa mvua
Katika msimu wa mvua, magonjwa mengi hutarajiwa, kwa hiyo viuavijasumu kama vile pen and strip, oxytetracycline 10% na gentamicin vinapaswa kutayarishwa.
Katika wiki ya pili ya msimu wa mvua, tumia dawa za kuua minyoo kwa sababu minyoo wengi huwa hai na huzaliana wakati mvua. Unaweza kudunga wanyama dawa ya minyoo kama vile bimectin na baada ya wiki nyingine moja, wape dawa ya kumeza kwa sababu wakati mwingine dawa za minyoo za sindano hazina nguvu dhidi ya minyoo maalum.
Ongeza nguvu ya dawa za kuua kupe kwa sababu kupe huwa nyingi katika msimu wa mvua, au unaweza kunyunyizia mara kadhaa.
Msimu wa kiangazi
Katika msimu wa kiangazi, suala la kawaida linaloathiri mbuzi ni viroboto. Hivi vinaweza kudhibitiwa kwa kuogesha mbuzi kwa sabuni, au kunyunyizia dawa za unga.