Kupandikiza ni mchakato wa kuhamisha mmea kutoka sehemu moja hadi nyingine, na kutunza miche katika mazingira salama.
Kupandikiza ni mchakato nyeti lakini hutoa faida nyingi kwa wakulima. Kutumia miche ni njia rahisi na ya kawaida ya kuanzisha kilimo cha mboga. Miche ni mbegu zilizoota.
Masharti
Wakati ufaao wa kupandikiza miche hutegemea ukuaji wa majani ya kweli yaliyotofauti na majani ya mapema. Kabla ya kupandikiza hakikisha udongo una ubora mzuri, na uwezo wa kushika unyevu.
Pandikiza miche alasiri ili kusaidia mmea kupona wakati wa kupandikiza.
Kuimarisha miche
Hapa ndipo unapoanza kuzoeza miche mazingira yao ya baadaye na ya kudumu. Ni hatua muhimu kwa mafanikio ya mmea.
Miche huhitaji muda ili kuzoea mazingira mapya kabla ya kupandikizwa. Kwa muda wa wiki moja hadi mbili, acha miche izoee mazingira mapya.
Kupandikiza
Tumia jembe, sepeto au mwiko kutengeneza shimo dogo shambani. Tengeneza mashimo kwa kina kulingana na mizizi ya mmea. Hakikisha kwamba mizizi imeshikiliana na udongo.
Weka mmea ndani ya shimo na ujaze nafasi iliyobaki na udongo wenye rutuba. Nyunyizia maji kwenye udongo uliozunguka mmea ili kuruhusu mizizi kufikia virutubisho.
Mshtuko wa kupandikiza
Ikiwa mmea utaanza kunyauka, au kugeuka na kuwa rangi ya manjano kutokana na jua kali, tolea mimea kivuli.