Pilipili hoho ni mboga inayokuzwa na kutumika kama viungo ulimwenguni kote. Inaweza kukuzwa kwa njia ya kawaida na kwa mchanganyiko wenye rutuba bila udongo (hydroponics).
Wakati wa kupanda pilipili hoho kwa njia ya hydroponic, fuatilia ukuaji wa zao kutoka kupandikiza hadi hatua ya maua, na kisha hadi hatua ya kukomaa. Baada ya kukomaa, vuna, ainisha na fungasha bidhaa ili kuichukua sokoni. Katika mfumo wa hydroponics, mirija ya kutonesha huwekwa kwenye vihori ili kuhakikisha kwamba mimea inapata maji yenye virutubisho vingi.
Faida za hydroponics
Pilipili hoho zikilimwa kwa njia ya hydroponics, huwa unaokoa ardhi inayohitajika, unaokoa maji kwa sababu kwa vile kuna uchakataji wa maji na virutubisho. Pia mahitaji ya wafanyikazi yanapunguzwa kwa kuwa hakuna haja ya kupalilia. Udhibiti wa wadudu na magonjwa unapungua kwa 80%, na hakuna haja ya kufanya mzunguko wa mazao.
Pilipili hoho iliyokuzwa kwa njia ya hydroponics ina ubora wa juu na maisha marefu ikilinganishwa na pilipili hoho ya kawaida. Hii ni kwa sababu kwamba, kwa kutumia njia ya hydroponics, pilipili hoho inaweza kupata virutubisho vyote vinavyohitajika kustawi. Kufunga pilipili hoho na karatasi ya plastiki huongeza maisha yake.
Ongezeko la thamani
Unaweza kuongeza thamani kwa nyanya za daraja la 3 au pilipili hoho ambazo haziwezi kufika sokoni. Bidhaa zilizoongezwa thamani zina maisha marefu na hupata thamani bora kwenye soko.
Pilipili hoho nyekundu inaweza kutumika kutengeneza mchuzi wa pasta, michuzi ya nyama nakadhalika.
Pilipili hoho ya manjano inaweza kuwekwa kwenye makopo au kubadilidhwa kuwa unga huku nyanya zinaweza kutumika kutengeneza mchuzi wa makopo.