Kwa vile maji ni tatizo kubwa linaloathiri uzalishaji wa mazao hasa wakati wa kiangazi, umwagiliaji kwa njia ya kutonesha ni suluhisho linalowezekana, kwani hutoa matumizi bora ya maji, hupunguza magonjwa, hupunguza mmomonyoko wa udongo na uchenjuaji wa madini.
Ni njia ya kutonesha maji polepole, yakielekezwa kwenye mmea.
Ujenzi wa mfumo
Tayarisha vitalu vilivyoinuliwa, weka pampu ya maji na tanki juu kwa urefu wa mita 1 – 2, ili maji yaweze kutiririka kwa urahisi. Weka kichujio ambacho husafishwa mara moja kwa wiki. Weka kipimo cha shinikizo kwenye mrija mkuu na unganisha mrija mkuu. Anzisha na usawazishe mirija ya kutonesha kwa kutumia mianzi au nyenzo zingine zinazopatikana.
Funga mrija wa kutonesha kwa kukunja mwishowe na urekebishe. Pitisha maji ndani ya miriji mara moja kwa mwezi ili kudumisha mfumo. Weka matandazo baada ya kuweka mfumo na unganisha mrija ya kutonesha kwenye mrija mkuu.
Hifadhi mfumo iwapo hautumiki na rekebisha tena nyenzo za mfumo mara tu zinapoharibika. Kagua shinikizo mwishoni mwa mrija wa kutonesha mara kwa mara, pamoja na mtiririko wa matone mara moja kwa wiki, na pandikiza miche karibu na mirija ya kutonesha.