»Jinsi ya kujenga banda la mbuzi lililoinuliwa»

3 / 5. 1

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=IwtOSC-e1CI

Muda: 

00:08:45
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Hamiisi Semanda

Banda linaweza kujengwa chini au kuinuliwa.

Banda lililoinuliwa ni ghali zaidi kuliko banda la chini kutokana na kiasi kikubwa cha mbao zinazohitajika katika ujenzi. Iwapo mfugajo ana miti yake na bei ya soko ni nafuu, ni bora kuitumia kujenga banda la mbuzi kuliko kuiuza kwa bei nafuu.

Umuhimu wa kuinua banda la mbuzi

Unapojenga banda la mbuzi lililoinuliwa, kunapaswa kuwa na nafasi zilizoachwa kati ya mbao za kutengeneza sakafu ili kuruhusu kinyesi na mkojo kupita. Ni makosa kujenga banda lililoinuliwa bila kuacha nafasi hiyo.

Ukiwa na banda la mbuzi lililoinuliwa, hauhitaji kulisafisha kila siku. Pia ikiwa wafanyakazi wako si wazuri katika usafi, ni bora ujenge banda lililoinuliwa.

Mazingatio ya banda lililoinuliwa

Unapojenja banda, hakikisha kwamba mbuzi wana eneo la kufanyia mazoezi.

Banda la mbuzi linapaswa kuwa mita 1.5 kutoka chini na pande zote ziwe zimefungwa ili kuzuia mbuzi kuingia chini ya banda kwenye kinyesi na mkojo. Urefu wa mita 1.5 kutoka chini unatosha kuruhusu mtu kuingia chini na kusafisha banda.

Katika banda lililoinuliwa, unaweza pia kuligawanya ili kuwa na zizi la watoto na sehemu zingine katika chumba hicho hicho. Unaweza pia kuitengeneza ili mbuzi wa sehemu tofauti waweze kutumia eneo moja la kunyunyiziwa dawa bila kuchanganyika pamoja.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:50Banda lililoinuliwa ni ghali zaidi kuliko banda la chini
00:5101:30Unapojenga banda la mbuzi lililoinuliwa, acha nafasi kati ya mbao za sakafu.
01:3102:15Ni makosa kujenga banda lililoinuliwa bila kuacha nafasi kwenye sakafu.
02:1603:15Hauhitaji kusafisha banda lililoinuliwa kila siku.
03:1603:19Unaweza kuligawanya katika maeneo mbalimbali.
03:2004:50Unaweza pia kuligawanya ili mbuzi wawe na eneo moja la kunyunyiziwa dawa bila kuchanganyika pamoja.
04:5106:00Unapojenja banda, hakikisha kwamba mbuzi wana eneo la kufanyia mazoezi.
06:0107:40Banda la mbuzi linapaswa kuwa mita 1.5 kutoka chini na pande zote ziwe zimefungwa.
07:4108:30Katika usimamizi wa mbuzi, hakikisha wanyama wako hai, ni aina bora. Pia wachanje na kuwanyunyizia dawa.
08:3108:45Hitimisho

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *