Sungura kuzaliana sana na sungura jike anaweza kuzaa hadi watoto 30 kwa mwaka ikiwa atatunzwa vizuri. Hata hivyo, kuzaliana kwa sungura hakutegemei tu kile wanachokula, pia wanahitaji matunzo mazuri na mbinu bora za kuzalina, na hivyo waweze kuuzwa kwa bei nzuri.
Uteuzi wa sungura kwa kuzaliana
Sungura dume anafaa kuwa na mapumbu yaliyostawi vizuri, na pia kuwa na afya nzuri pamoja na uwezo wa kufanya majukumu yake vizuri. Anafaa pia kuwa na umri wa miezi 6 hadi 8 na uzani wa 2 hadi 3 Kgs. Sungura jike anafaa kuwa na matiti 8, awe na afya nzuri na aweze kuzaa watoto wengi. Jike anafaa kuwa na umri wa miezi 6 hadi 7, na uzani angalau wa 2 Kgs.
Epuka kuwa na sungura dume na jike kutoka kwenye familia moja kwa sababu unaweza kuambulia matatizo ya utasa na ugumba pamoja na watoto walemavu. Ili kuepusha kupandana mapema, kutenganisha sungura dume na jike mara wanapofikisha miezi 3.
Afya ya sungura
Hakikisha kwamba sungura jike na dume wana afya njema. Badilisha dume wasiyofanya majukumu yao vizuri kwa wale wanaofanya kazi vizuri. Tenganisha dume wanaotoka kwa wakulima wengine ili kupunguza uwezekano wa kusambaza magonjwa. Sungura jike aliye na afya njema hutembea katika banda lake bila kuhara, wala hatakuwa na dalili za upele, au vimelea.
Kufanya sungura wapandane
Wakati uke wa sungura jike una rangi nyekundu, jike huyo huwa kwenye joto na anaweza kupandana na dume. Ili kufanya sungura wapandane, mpeleke jike kwenye banda la dume asubuhi au jioni. Jike aliye na uzoefu anafaa kupandana na dume asiyo na uzoefu.
Ikiwa jike hatakubali kupandwa, usimulazimishe laa sivyo uke wake unaweza kuharibiwa. Ikiwa jike atakubali, muache apandwe mara mbili kabla ya kumtoa kwenye banda ili kuongeza uwezekano wa kufanikiwa
Ukaguzi wa ujauzito
Angalia kama jike ameshika mimba baada ya siku 12 hadi 14 kwa kupima uzani wake, na kugusa tumbo la jike. Kuwa muangalifu ili usimguse sungura jike kwa nguvu au uchokozi kwa sababu unaweza kusababisha mimba kutoka. Siku ya kuzaa huandikwa kwenye karatasi ya kufuatilia.
Andaa sehemu ya kuzalia kabla ya jike huzaa. Sehemu ya kuzalia inafaa kusafishwa na kuwekewa dawa za kuua viini