Mbuzi kwa kawaida huonekana kuwa na afya bora wakati wa kiangazi kwanai hawashambuliwi sana na magonjwa, na nyasi wanazotumia huwa na unyevu kidogo.
Wakati wa msimu wa mvua, wakulima mara nyingi huingia gharama kubwa kwa dawa za kutibu magonjwa kama vile ugonjwa wa mapafu, kikohozi, na mafua, hasa kutokana na hali ya baridi na unyevunyevu. Kinga-mwili ya mbuzi huwa dhaifu katika kipindi hiki. Kwa hivyo, mbuzi huonekane kuwa hawana afya njema. Ili kupunguza changamoto hizo, wafugaji wa mbuzi wanapaswa kupunguza idadi ya mifugo ili kupunguza gharama za matibabu wakati wa mvua. Gharama hizi zinaweza kukidhiwa kwa kuuza mbuzi, kupata michango, au kuhamisha mifugo maeneo mengine. Zaidi ya hayo, wakulima wanapaswa kuhakikisha kuwa wamehifadhi dawa ya kutosha ili kukidhi mahitaji yao katika msimu mzima.
Chanja mbuzi wako dhidi ya magonjwa ya kawaida kama vile nimonia kabla ya msimu wa mvua kuanza . Wasiliana na daktari wako wa mifugo kwa ushauri wa kununua dawa kwa wingi kabla ya msimu wa mvua, jambo ambalo linaweza kusaidia kupunguza gharama. Kwa kuwa viini vya magonjwa, minyoo na mayai ya wadudu hupatikana zaidi wakati wa mvua, ni vyema kuchunga mbuzi katika maeneo ya juu wakati huu. Kitendo hiki kinapunguza uwezekano wa mbuzi kubeba vijidudu kwenye kwato zao, jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa kama vile kuhara, hasa kwa watoto.
Mambo zaidi juu ya Mbuzi
Ili kupunguza vifo na gharama za uzalishaji, tafuta mwongozo kutoka kwa wataalamu ili kusimiamia vizuri mifugo yako wakati wa msimu wa mvua. Tekeleza hatua za usafi kama vile kuwapa mbuzi mahali pa kuogeshea miguu wanaporudi kutoka kwenye shamba ili kuua vijidudu vinavyoweza kubeba kutoka shambani. Mara kwa mara safisha banda la mbuzi ili kudumisha mazingira safi na yenye afya.
Magonjwa yanapoendelea miongoni mwa mbuzi wako, ni vyema kuwatenganisha wanyama walioathirika badala ya kuwapeleka mashamba mengine. Hii husaidia kuzuia kuenea kwa magonjwa na kuhakikisha afya ya jumla ya kundi lako la mbuzi.