»Jinsi ya Kudunga Kuku na Chanjo ya mdondo(kideri) «

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=Vk0ADDcpvQM

Muda: 

00:12:39
Imetengenezwa ndani: 
2022

Imetayarishwa na: 

Africhic

Mdondo au kideri ni ugonjwa wa virusi ambao unaweza tu kudhibitiwa na si kutibiwa. Ugonjwa wa mdondo unaweza kudhibitiwa kwa kuwachanja ndege katika hatua tofauti.

Kuna aina mbili za chanjo: chanjo ya mdomoni, na chanjo ya lasota. Unapotumia chanjo ya mdomoni, changanya kipimo kwa kuvunja kifuniko cha chupa huku ukifungulia chanjo ndani ya maji. Tumia maji ambayo hayana klorini kwa ufanisi mzuri wa chanjo.

Chanjo ya Lasota

Chanjo ya Lasota hudungwa kwa kuku na hufanya kwa miezi sita bila ugonjwa wa kideri kutokea tena. Ili kuhifadhi chanjo kwa muda mrefu, weka chanjo kwenye jokofu, lakini usiigandishe.

Jinsi za kuchanja ndege

Unaweza kutumia sindano ya kawaida au sindano ya kiotomatiki.

Unapotumia sindano ya kiotomatiki, ingiza sindano ndani ya chupa ua chanjo, uiunganishe na kifaa cha ya kuchanjia. Tumia sindano ndogo kutoboa sehemu ya juu ya chupa ya chanjo ili kupitisha hewa.

Chukua sindano ambayo haijatumiwa na uifunge kwa ncha ya kifaa cha kuchanjia, na usome kipimo kabla ya kutumizi chanjo.

Sehemu za kudunga chanjo

Usimwage chanjo kwenye sakafu ili kuzuia kuenea kwa sehemu zingine za shamba. Unaweza kudunga ndege sindano katika sehemu mbili; matiti na mapaja. Dunga sindano kwa muinamo wa digrii 60, huku ukiepuka ncha ya sindano kugusa mfupa.

Unapomshikilia ndege wakati wa kumchanja, shikilia miguu kwa nguvu na utumie mkono wa kushoto kumshika ndege kwa mabega ili kuhisi sehemu ya matiti utakayodunga.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:30Mdondo au kideri ni ugonjwa wa virusi ambao unaweza tu kudhibitiwa na si kutibiwa
00:3101:01Ili kudhibiti kideri , wape ndege chanjo katika hatua tofauti.
01:0201:34Kuchanganya chanjo ya mdomoni.
01:3502:50Ili kuhifadhi chanjo kwa muda mrefu, weka chanjo kwenye jokofu
02:5104:20Chanjo ya Lasota hufanya miezi sita
04:2105:05Unaweza kutumia sindano ya kawaida au sindano ya kiotomatiki.
05:0605:36Unapotumia sindano ya kiotomatiki, ingiza sindano ndani ya chupa ua chanjo
05:3706:10Iunganishe na kifaa cha ya kuchanjia. Toboa sehemu ya juu ya chupa ya chanjo ili kupitisha hewa.
06:1106:41Chukua sindano ambayo haijatumiwa na uifunge kwa ncha ya kifaa cha kuchanjia
06:4207:30Soma kipimo kabla ya kutumizi chanjo.
07:3108:15Kudunga chanjo kunahitaji watu wawili.
08:1608:58Soma maagizo kabla ya kudunga chanjo.
08:5910:00Dunga sindano kwa paja , huku ukiepuka ncha ya sindano kugusa mfupa.
10:0111:13Unaweza pia kudunga chanjo kwenye sehemu ya matiti ya ndege
11:1412:39Unapomshughulikia ndege hakikisha usiwadhuru.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *