»Jinsi ya kuanzisha ufugaji wa kuku wa hariri «

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=cjmy8tDBrsg

Muda: 

00:04:58
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Business Ideas English

Kwa kuwa ni biashara nzuri, ubora wa wingi wa bidhaa za kuku wa hariri hutegemea mbinu za usimamizi zinazotumika.

Kuku wa hariri ni moja wa kuku maarufu na wanaopendwa zaidi, ni ndege wa kuburudisha na mapambo. Ufugaji wa kuku wa hariri huongeza faida za kiuchumi za wafugaji.

Usimamizi wa kuku

Kwa usimamizi na utunzaji sahihi, ufugaji wa kuku wa hariri ni biashara yenye faida. Anzisha biashara kwa kununua vifaranga bora, wenye afya njema na wasio na magonjwa. Tengeneza mabanda bora kulingana na pesa na vifaa vinavyopatikana. Unaweza kutumia zege au vifaa vya kienyeji kama vile miti ya mianzi kutengeneza banda.

Vile vile, dumisha mfumo mzuri wa uingizaji wa hewa ndani ya banda ili kuondoa hewa mbaya, na hivyo kulinda ndege dhidi ya magonjwa. Hakikisha kuna mwanga wa kutosha ndani ya banda, na pia safisha na kukausha banda vizuri. Tolea ndege nafasi ya kutosha , yaani futi 10 za mraba katika banda. Wape chakula bora ili kuboresha ukuaji na uzalishaji wa kuku. Kamwe usilishe kuku chakula kilichochafuliwa na kila mara watolee maji safi ya kutosha.

Fuga ndege kwa uwiano wa jogoo 1 kwa majike 10 kwa ajili ya ufugaji sahihi, na hakikisha kwamba kuku wanafugwa katika hali kavu kwani manyoya yao hayawezi kuzuia maji. Chanja ndege kwa wakati ufaao, na uendelee kuwasiliana na daktari wa mifugo.

Hatimaye fanya mikakati ya masoko kabla ya kuanza biashara.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:22Kuku wa hariri ni moja wa kuku maarufu na wanaopendwa zaidi.
00:2301:17Ni ndege wa kuburudisha na mapambo.
01:1802:05Nunua vifaranga bora, wenye afya njema na wasio na magonjwa. Tengeneza mabanda bora
02:0602:45Dumisha mfumo mzuri wa uingizaji wa hewa ndani ya banda. Hakikisha kuna mwanga wa kutosha.
02:4603:32Tolea ndege nafasi ya kutosha na chakula bora.
03:3303:46Kamwe usilishe kuku chakula kilichochafuliwa.
03:4704:18Fuga ndege kwa uwiano wa jogoo 1 kwa majike 10, na hakikisha kwamba kuku wanafugwa katika hali kavu.
04:1904:35Chanja ndege kwa wakati ufaao, na uendelee kuwasiliana na daktari wa mifugo.
04:3604:44Hatimaye fanya mikakati ya masoko kabla ya kuanza biashara.
04:4504:58Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *