Ufugaji wa kuku duniani kote ni chanzo kikubwa cha protini na kipato. Hata hivyo, kabla ya kuanza ni muhimu kupata taarifa sahihi na kunakili wafugaji waliofaulu.
Tambua aina ya ndege unaohitaji na ufuate hatua bora za ufugaji kama vile, kutolea ndege milisho bora, na kuelewa biashara vizuri ili kupata uzoefu zaidi.
Hatua za kufuata kwa wafugaji wanaoanza
Anza kwa kuomba mkopo, kwani ufugaji wa kuku unahitaji uwekezaji mwanzoni.
Pata vifaranga kutoka kwa wauzaji wanaoaminika. Hata hivyo, kila mara anza na idadi ndogo ya ndege ambayo itagharimu pesa kidogo.
Tambua aina ya kuku utakayofuga, yaani kuku wa nyama au wa mmayai. Kisha uza bidhaa zako za kuku au ili kupata pesa.
Hakikisha unachagua eneo zuri la shamba ili kurahisisha usafiri, na kuepuka malalamiko kutoka kwa jamii.
Pia jenga banda zuri la kuku kulingana na aina ya ndege kwani nyumba kubwa ni nzuri kwa wazalishaji wa kibiashara.
Nunua vifaa sahihi kama vile vihori vya maji na chakula. Daima epuka kuajiri wafanyikazi wengi kwani hii inahitaji pesa zaidi.
Andaa eneo pa kutotoleshea vifaranga kabla ya kuwaleta. Hakikisha usimamizi mzuri wa afya kwa kuchanja ndege na kuwatolea chakula bora na maji safi.
Mwisho, tumia mbinu sahihi za uuzaji kama vile kufanya utafiti ili kuongeza uuzaji wa bidhaa za kuku kwa ajili ya kuongeza kipato.