»Jinsi ya kuanzisha ufugaji huria wa kuku«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=Fandq738V5U

Muda: 

00:12:30
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

AfriChic

Ufugaji huria ni mradi mzuri kwa wafugaji wengi. Ili kuanzisha mradi huo unahitaji kuwa na ardhi ya kutosha.

Eneo la kufugia kuku lazima lifungwe na uzio kwa pande zote. Katika eneo la mlango wa banda, weka dawa ya kuua viini ili itumike kwa miguu kabla ya kuingia. Hii ni kwa ajili ya hudhibiti kuku dhidi ya magonjwa.

Banda la kuku

Banda la kuku linapaswa kuwa na mfumo mzuri wa kuondoa maji wakati kuna mvua nyingi. Maranda ya mbao yanaweza kutumika kama matandiko ya kuku. Hii husaidia kudhibiti kuku dhidi ya vijidudu, magonjwa na kinyesi chao.

Banda la kuku lazima lisiingize panya na mikoko. Wape ndege uwanja wa kutosha kuchezea, na pia udumishe usafi ndani na nje ya banda.

Kulisha kuku

Epuka kuweka malisho ndani ya banda, kuku wanapaswa kulishiwa nje. Kuku wawe na banda la kutosha, sehemu ya kupumzikia na eneo la kutaga mayai. Tumia chombo cha kunyweshea kilicho na mkono juu. Kamba hufungwa kwenye chombo cha kunyweshea na kuning‘inizwa ili maji yasimwagike.

Chombo cha kulishia na kunyweshea kinafaa kuinuliwe kidogo ili kuku wapate chakula kwa urahisi. Ndege wa porini lazima wafukuzwe kwani wanaweza kuleta magonjwa.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:00Ili kuanzisha mradi huo unahitaji kuwa na ardhi ya kutosha
01:0101:28Katika eneo la mlango wa banda, weka dawa ya kuua viini kabla ya kuingia
01:2902:22Pumba za mbao zinaweza kutumika kama matandiko ya kuku
02:2303:28Banda la kuku lazima lisingize panya na mikoko
03:2904:50Epuka kuweka vifaa vya kulishia ndani ya banda
04:5105:47Kuku lazima wawe na banda la kutosha
05:4806:28Nunua chombo cha kunyweshea kilicho na mkono juu ambapo kinaweza kuning‘inizwa na hivyo kurahisishia kuku kunywa
06:2907:17Chombo cha kulishia kinafaa kuinuliwe kidogo ili kuku wapate chakula kwa urahisi.
07:1808:01Ndege wa porini lazima wafukuzwe kwani wanaweza kuleta magonjwa.
09:00012:30Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *