Biashara ya ufugaji wa nguruwe huleta mapato ya haraka kwa vile dume hukomaa katika miezi 18, na jike ana muda wa ujauzito usiozidi siku 115. Nyama ya nguruwe huliwa sana.
Nguruwe huhitaji utunzaji na usimamizi bora. Mambo muhimu ya kuzingatia katika ufugaji wa nguruwe ni pamoja na ardhi, mtaji, na soko. Kuna njia mbili za ufugaji wa nguruwe, na hizi ni; mbinu ya banda na mbinu huria. Samadi ya nguruwe ni mbolea bora kwa wakulima na pia hutoa malisho kwa samaki.
Hatua za kuanzisha ufugaji wa nguruwe
Anza kwa kuchagua mbinu ya ufugaji wa nguruwe,eneo pa kuwafugia, idadi ya nguruwe wa kufugwa na lengo la soko. Fanya utafiti wa soko, uchanganuzi wa faida na gharama, na kisha andika mpango wa biashara.
Jenga banda ili kutoa kivuli kwa kuwa halijoto husababisha changamoto kubwa kwa wafugaji wa nguruwe
Hakikisha kwamba kuna hatua za kuzuia uenezaji wa magonjwa kutoka kwa mazingira ya nje. Lisha nguruwe chakula chenye lishe kilichochachushwa kwa siku 3.
Hakikisha unachachusha chakula cha nguruwe kwa vile kina afya zaidi kuliko chakula kikavu.
Hakikisha kuna kuna vifaa vya kupoesha na kuburudisha halijoto kwa kuwa nguruwe hawana tezi za jasho. Ondoa samadi ipasavyo ili kudhibiti magonjwa.
Hakikisha kuna makazi yanayofaa na uingizaji mzuri wa hewa ili kudhibiti hali mbaya ya hewa. Ruhusu nguruwe kulisha kwenye malisho ya majani.
Pia epuka kuchanganya nguruwe wa umri tofauti ili kupunguza kupigana.
Hatimaye, wasiliana na daktari wa mifugo iwapo kuna dalili za ugonjwa ili kutoa dawa haraka.