Ufugaji wa samaki unatekelezwa na wafugaji wengi duniani kote kwa sababu ya faida zake kubwa. Hata hivyo, usiweke samaki wachanga kwenye bwawa kuzidi kiwango kinachopendekezwa ili kuhimiza ukuaji sahihi.
Wakati wa kulisha samaki, malisho mengi yakionekana yanaelea juu ya maji huwa ishara kwamba samaki wamelishwa kupita kiasi, na huku kunaweza kusababisha uchafuzi wa maji. Maji yanapaswa kubadilishwa mara kwa mara. Kwa mfano kwa mabwawa ya turubai ya saruji, maji yanapaswa kubadilishwa kila baada ya siku 3–4, na kwa mabwawa ya udongo maji yanapaswa kubadilishwa mara moja kwa mwezi.
Hatua za uzalishaji wa samaki
Kwanza tafuta na ufuge aina bora ya samaki kutoka kwenye wafugaji wa samaki wanaoaminika ili kutopewa aina duni za samaki zinazoshambuliwa na magonjwa. Lazima uwalishe samaki vizuri kila mara ili kupata faida nzuri. Vile vile tumia vyakula vilivyopendekezwa mwanzoni kwa ukuaji wa haraka wa samaki, na usizidishe wingi wa samaki katika bwawa.
Ulishaji wa samaki ufanyike asubuhi na jioni huku ukihakikisha kuwa wanalishwa vizuri, kwani vyakula vya ziada vilivyobaki kwenye bwawa bila kuliwa huchafua maji na mazingira. Unapaswa pia kudumisha mazingira safi kwa kubadilisha maji mara kwa mara, na kuondoa maiti za samaki waliokufa mara tu wanapoonekana, kwani maji machafu hueneza magonjwa kwenye bwawa.
Kwa mfugaji mpya, unapaswa kuanza na samaki wachanga 400–500, pamoja na mtaji wa kutosha ambao unaweza kutumika kulipia gharama za; ardhi, ujenzi, malisho, samaki wachanga, vifaa, dawa na usafirishaji.
Faida za ugugaji wa samaki
Ufugaji wa samaki una faida kadhaa na hizi ni; samaki hutoa kipato kikubwa, na huhitajika sana kwa soko la ndani na nje ya nchi. Ufuhaji wa samaki ni rahisi kuanzishwa na kushughulikia.