Uvuvi unahusisha ufugaji wa wanyama wa majini kama samaki, kamba, uduvi na salmoni. Ni mradi wa faida sana kwa wafugaji ikiwa unafanywa vizuri.
Kuna aina tofauti za mabwawa ya samaki ambayo hutumiwa katika ufugaji wa samaki, haya ni pamoja na mabwawa ya udongo, mabwawa ya saruji, na mabwawa ya turubai. Hata hivyo, mabwawa ya turubai ni ghali na yana faida kwa vile yanaweza kuhamishwa kwa urahisi kutoka sehemu moja hadi jingine. Kwa upande mwingine, mabwawa ya saruji yanapendekezwa kwa vile yanaweza kusafishwa na kwa urahisi.
Ufugaji wa samaki wenye mafanikio
Anza kwa kujielimisha kuhusu ufugaji wa samaki kutoka kwa wafugaji wataalamu ili kupata na elimu ya kimsingi ya ufugaji wa samaki. Amua eneo pakuanzisha ufugaji wa samaki, kwani hii huamua aina ya bwawa litakalojengwa. Kwa mfano mabwawa ya udongo yanahitaji udongo wenye kiwango cha juu cha maji, na bora yawekwe kwenye udongo wa mfinyanzi au tifutifu. Mabwawa ya saruji au turubai yanahitaji kujengwa karibu na chanzo cha maji kwa vile huwa yanahitaji mabadilisho ya maji ya mara kwa mara.
Chagua eneo na angalia aina ya udongo ambao lazima uwe udongo wa mfinyanzi kwa vile unahifadhi maji. Pima pH ya maji ili kujua kama ni tindikali au alkali na uirekebishe ipaswavyo. Baada ya ujenzi, bwawa linapaswa kutibiwa na kuongezwa mbolea ili kudhibiti maambuki ya magonjwa, pamoja na kuongeza ukuaji wa chakula cha samaki.
Mwisho baada ya kujenga bwawa la samaki hakikisha kuna mabomba, mifuniko, nyavu, mifuko ya mchanga kwenye bwawa ili kuwezesha kujaza na kuondoa maji, pamoja na kuwalinda samaki dhidi ya wawindaji.