Migomba hulimwa sana, na mara nyingi huliwa kama kitindamlo. Uandaji t mzuri wa shamba wakati wa upandaji ni muhimu ili kupata mavuno bora.
Katika utayarishaji wa shamba, fyeka vichaka na uache baadhi ya miti ili ifanye kama vizuizi vya upepo kunapokuwa na hali mbaya ya hewa. Acha manyasi yakauke na kisha uyachome. Ardhi ambayo haijawahi kulimwa awali ina rutuba ya kiasili, na hivyo hakuna haja ya kuweka samadi wakati wa kupanda.
Usimamizi wa migomba
Anzisha shamba lako la migomba katika eneo lililo karibu na chanzo cha maji ili uwe na maji ya umwagiliaji endapo kutakuwa na haja. Ikiwa eneo hilo lina maji ya ziada, chimba mifereji ya maji shambani. Hii huzuia mafuriko ya shamba.
Miezi mitatu baada ya kupanda, weka samadi ya kuku ili kutoa virutubisho.
Ondoa machipukizi ya migomba ya ziadi ili kuzuia ushindani wa maji na virutubisho unaosababisha mimea kudumaa. Machipukizi ya migomba yaliyoondolewa yanaweza kupandwa mahali pengine na hivyo kuongeza idadi ya migomba.
Ikiwa una pesa walaki hauna muda, unaweza kuwekeza katika kilimo kupitia makampuni yanayoaminika. Haya yanaweza kukusaidia katika usimamizi wa shamba lako.