Usimamizi wa wivavi hariri
Kwa vile mboji ya kikaboni hutengenezwa na kutumika katika kilimo-hai, mkulima anapaswa kupanda takribani miti 500-1000 ya mnyonyo kwa ajili ya kulisha viwavi hariri. Baada ya miezi sita, atengeneze chumba cha unene ulio kati ya 12-20ft ili kufuga takiribani viwavi hariri 40000-80000. Wafundishe wafanyikazi juu ya usimamizi mzuri wa chumba cha viwavi, pamoja na kudumisha usafi ndani ya vyumba.
Vile vile, nunua mayai na uyaangue na uzingatie hatua za ukuaji wa viwavi hariri, tabia zao. Hakikisha kwamba unalishe viwavi kwa muda wa siku 3. viwavi hariri huhitaji mazingira safi, na pia watenganishe ili kupunguza msongo.
Tibu viwavi hariri kwa kueneza chokaa wakati wamelala na punguza idadi ya watu wanaoingia ndani ya chumba cha viwavi ili kuzuia kuenea magonjwa. Dhibiti halijoto ndani ya chumba kwani linapaswa kuwa kati ya nyuzi joto 24-50 sentigredi. Viwavi hariri wanapaswa kumaliza mzunguko wao wa maisha ndani ya siku 28.