Mahindi ni zao kuu la chakula na biashara kwa wakulima wengi, hata hivyo kujifunza hatua za uzalishaji na utumiaji wa mbolea ya majani na mbolea ya madini huwasaidia wakulima kuongeza mavuno ya mahindi.
Daima epuka udongo wa kichanga, changarawe na udongo usio na kina kirefu, kwani huzuia ukuaji wa mahindi. Kuna zana nyingi za kupanda mahindi kama vile kisu, na jembe la kuchimba mashimo.
Mchanganyiko wa mbolea za majani na mbolea za madini huongeza mavuno ya mahindi.
Hatua za Uzalishaji
Chagua eneo lenye udongo ulio na rutuba na kina kirefu, na ulime au tumia kemikali kuondoa magugu na kulainisha udongo kabla ya kupanda.
Kisha chagua aina bora ya mbegu ambayo hukomaa ndani ya muda mfupi ili kupata mavuno mengi. Panda katikaka msimu wa upanzi unaopendekezwa.
Pima uotaji wa mbegu ukitumia mbegu zilizoidhinishwa kwa kuhesabu, kupanda na kumwagilia mbegu mia moja zilizothibitishwa.
Panda mbegu kwa kuzingatia matokeo ya vipimo vya uotaji; kati ya 85% – 100% panda mbegu 2, 70% – 84% panda mbegu 3, 50% – 70% panda mbegu 4 au pata mbegu bora, na 0 – 50% pata mbegu mpya.
Panda kwa safu ukizingatia muachano wa 80cm kati ya safu na 40cm ndani ya safu katika kina cha 5–7 cm huku ukitumia zana zinazofaa.
Mbolea za majani na mbolea za madini
Weka mbolea ya NPK yenye uzito wa kilo 100 kwa ekari moja kwa kutengeneza mashimo kwa sentimita 5 kutoka kwenye msingi wa mimea katika wiki ya kwanza.
Katika wiki ya pili, weka 250ml ya kianzio cha mahindi kwa ekari moja, yaani 50ml bomba la kunyunyizia dawa ambalo huchukua lita 15.
Pima kwa ukamilifu 25ml ya kianzio cha mahindi na mimina katika kinyunyizio cha lita 15 kilichojazwa nusu na maji, funga na tikisa vizuri ili kuchanganyika vyema. Kisha jaza bomba na maji.