Mpunga uliokaushwa vibaya hukabiliwa na ukungu na wadudu, na hivyo kusababisha hasara. Ukaushaji wa mpunga ni mgumu haswa wakati wa mvua na mawingu, kwa hivyo unahitaji kutumia kifaa cha kukausha.
Kutumia kikaushio cha BAU-STR kukauka mpunga hupunguza gharama za vibarua na hatari za kiafya. Kikaushio cha BAU-STR kinajumuisha kipulizia, pipa la ndani, pipa la nje, bomba la kupitisha hewa moto na jiko. Pipa la ndani na pipa la nje hukaa kwenye sakafu yoyote tambarare, kipulizia huwekwa kwenye pipa la ndani, jiko huwekwa kando ya pipa lingine na bomba la kupitisha hewa moto huunganisha jiko na kipulizia.
Vyanzo vya moto na nishati za kuendesha kikaushio
Nafaka zinapaswa kuwekwa sawasawa katika nafasi tupu kati ya pipa la ndani, damani ya plastiki hutumika kufunika sehemu ya juu ili kuzuia hewa ya moto kuvuja nje. mkaa wa maganda ya mpunga hukatwa katika vipande vidogo vya urefu wa sentimeta 2.5 ambavyo hutumika kama chanzo cha moto jikoni, na umeme au jenereta hutumika kuendesha kipulizia. Kipulizia hufyonza hewa moto kutoka jikoni kupitia bomba la chuma na kupuliza hewa ndani ya pipa la ndani. Hii hukausha mpunga.
Joto linalopulizwa kwenye mpunga lisizidi nyuzi joto 43 kwa mupunga wa kutumika kama mbegu, na nyuzi 50 kwa mchele wa kuliwa. Ili kuwa mpunga bora, acha kwa muda wa masaa 4 hadi 5 baada ya kukauka.