Mbinu hizi ni pamoja na:
1. Ukuzaji wa Ujuzi wa Wakulima: Wakulima hupata mbinu muhimu kupitia mafunzo. Mafunzo haya yanajumuisha; ukomavu wa mazao, utafutaji wa soko, na usaidizi wa vikundi katika kuwawakilisha wakulima binafsi.
2. Kujiunga na Kikundi cha Kilimo: Kutoleana habari kuhusu jinsi ya kujiunga na kikundi cha wakulima karanga.
3. Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa: Mikakati madhubuti ya kudhibiti wadudu na magonjwa shambani inajadiliwa, ikisisitiza mbinu rafiki kwa mazingira.
4. Kuelimisha Jamii: Jamii inaelimishwa na kuhimizwa kushiriki katika kilimo cha karanga, pamoja na usambazaji wa miche kwa ajili ya mipango mipya ya kilimo.
5. Kupunguza madharaya mabadiliko ya hali ya Hewa: Mbinu za kukabiliana na hali mbaya ya hewa hufundishwa, kwa kuzingatia mbinu za umwagiliaji.
Kulima Aina mbalimbali za Karanga
Kuna aina tatu kuu za karanga katika kitengo hiki: Serenut 14R, Naronut 1R, Serenut 11T, Serenut 9T, na Serenut 8R. Aina hizi hutofautiana katika sifa na viwango vya ukomavu. Inashauriwa kupanda kila aina mara tatu ili kudumisha ubora wa mbegu. Muachano kati ya mimea unapaswa kuwa takriban sm 50 kati ya safu na sm 15 kati ya mimea, hivyo kusababisha kupanda takiriban mimea 26,000 kwa ekari.
Ili kudhibiti wadudu na magonjwa, dawa za kemikali mbazo haziathiri mazingira zinaweza kutumika. Ongezeko la thamani linawezekana kupitia uzalishaji wa karanga zilizofungashwa tayari, na kuzifanya zifikikie wateja kwa urahisi.