Faida na vidokezo vya upunguzaji wa miti

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=ndZTYCq0jHc&t=205s

Muda: 

00:04:06
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

West Multnomah SWCD

Upunguzaji wa miti ni mchakato wa kuchagua na kuondoa miti msituni.

Upunguzaji wa miti ni
muhimu katika usimamizi wa misitu. Hata hivyo, ni muhimu kujua kwa nini kitendo hicho hufanywa
na mambo yanayoathiri uchaguzi wa miti itakayokatwa. Wakati msitu wako hauna
mimea mingine ardhini, inashauriwa upunguze miti kwaani huku kunamaanisha kuwa matawi ni
manene sana na hayaruhusi mwanga wa jua kupenya
.

Wakati sahihi wa kupunguza miti

IIkiwa kuna miti ambayo ina mashina
madogo na matawi machache, inashauriwa uikate.

Unaweza pia kutembea kwenye msitu wako huku ukipima vipenyo vya mashina ili
kujua iwapo msitu wako ni mnene. Vipimo hivyo vinaweza kulinganishwa na vipimo
maalum vilivyotolewa katika machapisho ya ugani wa misitu.

Miti inaweza kukuzwa kati ya
miaka 10 hadi 15 na kisha
  yote hukatwa
mara moja, au ukaguzi wa mara kwa mara unaweza kufanywa ili kuondoa miti
iliyoharibika na isiyoweza kuuzwa.


Kanuni ya jumla wakati unapunguza
miti ni kwamba uondoe miti nyembamba na kuacha miti mikubwa kwa sababu miti
mikubwa huchukuliwa kuwa na afya zaidi kuliko miti nyembamba.


Umuhimu wa kupunguza miti

Kupunguza miti hutoa nafasi ya
kutosha na virutubishi ambavyo husababisha ukuaji bora wa miti iliyobaki.

 

Huongeza upenyaji wa mwanga wa
jua ambao huhimiza ukuaji wa mimea zaidi ardhini mwa msitu, na hivyo
kuongeza  anuai kadhaa za mfumo ikolojia.

 

Kupunguza miti huunda msitu wenye afya na kuboresha makazi ya
wanyamapori
.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:23Kujua kanuni bora za uchaguzi wakati wa kupunguza miti ni muhimu katika usimamizi wa misitu.
00:2400:44Ishara zinazoonyesha kwamba unahitaji kupunguza miti katika msitu wako.
00:4501:06Miti inaweza kukuzwa kati ya miaka 10 hadi 15 na kisha yote hukatwa mara moja
01:0701:35Ondoa miti nyembamba na uache miti mikubwa
01:3604:40 Umuhimu wa kupunguza miti
04:4104:46sifa

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *