Usimamizi wa ardhi
Kwanza, pima kiwango cha unyevu kilicho katika inchi 6 chini ya udongo kwa kutumia kipima unyevu. Udongo huhitaji angalau 60% na 80% ya unyevu. Mwagilia kwa muda maalum na pima viwango vya unyevu. Ongeza muda wa kumwagilia maji wakati unyevu wa udongo uko chini ya 50% baada ya siku 1 ya kumwagilia. Mwagilia maji mara kwa mara wakati hali ya hewa ni ya joto, na mwagilia kidogo wakati wa baridi.
Vile vile, mwagilia mazao kutoka chia ya ardhi na sio kutoka juu ili kuzuia kueneza magonjwa ya ukungu. Mwagilia kutegemea na aina ya mimea inayopandwa shambani kwani mimea tofauti na mahitaji tofauti ya maji.