Kutumia viuatilifu vya kemikali ni ghali, na ni hatari kwa watu na mazingira. Viuatilifu huua wadudu wenye manufaa ambao hula na kuua wadudu waharibifu. Viuatilifu pia huathiri udongo na maji.
Dawa asili zina vyanzo vya asili ambavyo vinadhibiti wadudu waharibifu, na ni rahisi kutumia, ni bei nafuu, na haziachi mabaki kwenye mimea. Dawa hizi zinafaa kutumiwa tu wakati zinahitajika na kwenye mimea iliyovamiwa na wadudu.
Faida za dawa asili
Majani ya mwarobaini yana dawa za asili ambazo hufanya mimea kuwa na ladha mbaya na hivyo huzuia mimea kuliwa na wadudu kama vile vidukari, nzi weupe na vipeperushi wa mimea.
Mimea hufyonza dondoo ya mwarobaini kupitia majani na mizizi na hivyo kuwadhibiti dumuzi ambao hula matawi ya ndani na mara nyingi hawaathiriwi na dawa ambazo hufikia tu sehemu ya nje ya mmea.
Dawa asili haziathiri wadudu wenye manufaa, wala mazingira kwani huoza kiasili.
Jinsi ya kuandaa dondoa
Kusanya matunda ya mwarobaini yaliyoiva kabisa ambayo yana rangi ya manjano au yale ya hudhurungi yaliyoanguka chini.
Loweka matunda ya mwarobaini kwenye maji kwa masaa 24 na uondoe maganda. Tandaza mbegu kwenye mkeka hadi zitakapokauka. Maganda yanaweza kutumika kwenye mbolea.
Matumizi ya dondoo la mwarobaini
Ili kuandaa dodoo ya kiini cha mbegu za mwarobaini, saga 5 kgs za mbegu hadi ziwe unga huku ukifunika pua yako kuzuia kichefuchefu au kutapika. Changanya unga kwa lita 10 za maji. Kwa ufanisi mzuri, ongeza vijiko 20 vya unga wa sabuni asili ili kuwezesha mchanganyiko kunata kwa mimea.
Weka mchanganyiko kwenye kivuli kwa masaa 24. Baada ya masaa 24 koroga mchanganyiko na uchuje mara 2 hadi 3. Tumia kitambaa cha pamba iwapo unachuja ili kuzuia chembechembe kuziba ncha ya bomba la dawa.
Nyunyiza mchanganyiko kabla ya mmea kutoa maua au wakati maganda yanatengenezwa. Athari zinaweza kuonekana baada ya siku 7 hadi 10. Katika msimu wa mvua, nyunyiza mchanganyiko mara nyingi.