Uvimbe wa kiwele ni maambukizi au ugonjwa unaofanya kiwele kuwa kigumu na kuvimba, na hivyo ng‘ombe hataki kukamuliwa.
Matumizi ya viuatilifu kwa muda mrefu sio mzuri kwa ng‘ombe. Viuatilifu huathiri maziwa na nyama ambayo sio nzuri kwa matumizi ya binadamu.
Kuzuia
Njia bora ya kuzuia uvimbe wa kiwele ni kudumisha usafi katika zizi la ng‘ombe na eneo la banda la ng‘ombe. Ondoa samadi na chakula kilicho mwagika kwenye zizi. Andaa eneo la kukamua na eneo la kupumzika ili kudumisha usafi.
Osha mikono yako na maji safi kabla na kati ya kukamua wanyama tofauti.
Safisha kiwele kwa maji safi na kukifuta kwa kitambaa safi kabla na baada ya kukamua.
Matibabu
Pima maziwa ya ng‘ombe mara kwa mara, na utibu ng‘ombe mara tu utakapoona dalili za uvimbe wa kiwele.
Kagua ubora wa maziwa. Tumia kifaa cha kukagua uwepo wa uvimbe wa kiwele.
Iwapo utatumia vifa maalum cha kukamua maziwa, tumia plag moja tu kwa kila titi.
Kamua maziwa yote yaliyo kiweleni, laa sivyo viini na vijidudu vinaweza kukua katika maziwa yaliyosalia.
Kufuta kiwele na maji ya uvuguvugu yaliyochemshwa na majani ya mpeera na mwarobaini.
Paka kiwele kilichoathiriwa na mchanganyiko wa kafuri na unga wa samuli kwenye mafuta baada ya kukamua.
Iwapo mnyama hajapata nafuu baada ya kutumia dawa ya mitishamba, basi wasiliana na daktari wako wa mifugo.