Mimea huhitaji maji ili kukua vizuri, lakini katika sehemu nyingi za ulimwengu, ardhi hujaa na mafuriko kwa muda mrefu. Tunaweza kupanda mazao kwenye vitalu au bustani zinazoelea, ambazo hutengenezwa kwa mimea inayooza kubadilika kuwa mbolea.
Vitalu hivi vinaweza kutengenezwa kwenye ziwa, mito na vyanzo vya maji ya msimu. Kwa kupanda vitalu vinavyoelea, tunaweza kupata mavuno mengi bila kutumia mbolea za madini na viuatilifu. Ili kutengeneza bustani inayoelea, unahitaji jahazi, ufito urefu wa mianzi na kijiti kilicho na ndoano. Awali, chagua eneo lenye angalau urefu wa maji wa mita 1 kwa kina, na gugu-maji lingi katika msimu wa mvua. Weka fito la mianzi juu ya gugu-maji, na ulivute kutoka pande zote mbili hadi kwenye fito la mianzi, na ulishindilie kwa miguu yako.
Ujenzi juu ya maji
Weka majani ya gugu-maji yakielekea katikati, na mizizi yake yakiagalia juu ili kurahisisha kuoza. Endelea kuongeza gugu-maji hadi chelezo cha magogo kitakapokuwa kigumu kutembea juu yake. Ondoa fito la mianzi chini ya chelezo ili uweze kulitumia tena. Acha tungamo la gugu litulie juu ya maji, na lipungue. Baada ya siku 7 hadi 10, na uongeze gugu-maji lingine juu ya chelezo.
Wakati unapoanza kutengeneza bustani inayoelea, pia anza kuandaa mipira ya mbolea oza. Mipira hii hutengenezwa kwa kuondoa maji kwenye gugu-maji lililooza. Panda mbegu kwenye mipira ya mbolea na kisha uzifunike. Mbegu huota kwa siku 2 hadi 3. Pandikiza miche siku 10 baada ya kuota kwenye kitalu kinachoelea.
Kupanda juu ya maji
Tengeneza mashimo ya kupandia kwa muachano wa 25cm. Weka mbolea kwenye mashimo haya na uweke ndani mwa shimo mipira pamoja na miche. Baada ya siku 15, ondoa mbolea kwenye kingo za kitalu kinachoelea. Weka mbolea kando ya kila mmea ili kuimarisha mimea na kuongeza madini.
Mwagilia kitalu ikiwa kuna jua kali na wakati kitalu kimekauka. Mboga zinazopandwa kwenye kitalu kinachoelea ni pamoja na Bamia, tango, kibuyu, malenge, maharagwe, tamarack na mchicha.
Changamoto kubwa katika vitalu vinavyoelea ni panya, lakini manufaa ni nyingi kuliko changamoto. Katika mwisho wa msimu wa kukuza mimea, songeza kitalu kwenye maji ya kina kifupi. Vunja vunja kitalu na ukitandaze shambani halafu, uhifadhi mbolea ya kutengeneza mipira mwaka ujao.