Minyoo wana faida kwa ukuaji wa mimea na kutengeneza mbolea oza, ambayo husaidia kukuza mimea kwa haraka. Kutengeneza mbolea ni rahisi na inaweza kufanywa kwa muda mfupi zaidi kwa hivyo, kuongeza mapato.
Minyoo hutengeneza mianya ambayo husaidia kulowesha maji udongoni, kuongeza unyevu, kupenya kwa mizizi. Mianya pia huruhusu mizizi ya mimea kufika chini zaidi kwenye udongo na kupokea virutubisho zaidi. Minyoo pia husaidia mbolea kuoza kwa haraka, kupunguza gharama ya mbolea, na kufanya mbolea iwe rahisi kutengeneza.
Kutengeneza mbolea oza
Chimba shimo umbo la mduara la kina cha urefu wa vidole 8, palipo na kivuli ili kuzuia mvua na jua. Weka plastiki ndani ya duara, kisha weka mviringo wa saruji juu. Plastiki hulinda mbolea dhidi ya unyevu ambao kwamba unaweza kusababisha uharibifu wa mbolea na minyoo kufa. Ongeza kikapu kimoja cha mchanga ndani ya mviringo na ueneze pande zote. Kisha weka kikapu kimoja cha matofali yaliyovunjika, na kimoja cha mchanga. Weka kikapu cha vipande vya mizizi ya ndizi. Kisha, weka kikapu cha samadi ng‘ombe na urudie tabaka mbili za mwisho. Chimba shimo ndogo katikati ya sehemu ya juu, weka ndani yake mkono mmoja wa minyoo, na zifunika kwa samadi. Nyunyiza maji ya kutosha juu, na funika mviringo kwa plastiki ili kutoa mazingira mazuri kwa minyoo. Mwishowe, baada ya wiki 3–4 mbolea itakua tayari kutumi. Wakati wa maadalizi ya shamba,ongeza mbolea hii kwa udongo ili kudumisha rutuba ya udongo.