Viungo vimekua sehemu ya historia ya wanadamu na ardhi ziligunduliwa katika pilkapilka ya kutafuta viungo. Viungo ni bidhaa ndogo, lakini umuhimu wake kwa upishi kimsingi una thamani.
Viungo vitano vya bei ghali zaidi ulimwenguni ni; mdalasini, karafuu, iliki, vanila na safroni .Mdalasini unagharimu dola 6 kwa paundi na inatokana kutoka gome la mdalasini na asili ya india. Kiungo cha karafuu kinagharimu dola 7–10 kwa paundi na ni asili ya Indonesia. Karafuu inaongeza ladha kwa vinywaji kama kahawa, kokoa ya moto na mvinyo.Karafuu ina harufu na ladha tofauti, na ni dawa kwa maradhi mengi na ni kiungo cha manukato na harafu zingine.
Iliki
Iliki inagharimu dola 30 kwa paundi na ladha yake ina nguvu sana. Ni asili ya India na inakuja katika aina mbili tofauti, iliki nyeusi au kijani. Iliki tunayo shirikiana sana kwa jina na ladha ni iliki ya kijani. liki nyeusi ina ladha minti na harufu ya moshi ukilinganisha na iliki ya kijani.
Safroni
Safroni inagharimu dola 1600–5000 kwa paundi. Safroni Inatoka kwa maua fulani ambayo ni ya asili ya Asia ya Kati na hii ndio sababu yake kuwa ghali sana. Kiungo chenyewe ni maua ya kike na kila ua ina sehemu tatu pekee ya kike. Ili kupata safroni unahitaji maua takriban 80,000. Nyongeza ya safroni kwa chakukla huleta ladha tamu na rangi kama hakuna viungo vingine kama hivyo.
Maelezo Zaidi
Kiungo ya Safron kawaida huleta ladha ya dhahabu- manjano ambayo ni ya kupendeza kama jua. Viungo haswa vilivyotengenezwa kutoka kwa mbegu ya safroni vina sehemu kubwa za mafuta, protini na kabohaidreti. Mwishowe, viungo vya vanila hugharimu kati ya dola 50– 200 kwa paundi. Unahitaji tu viungo kidogo ili kupata ladha kwa sababu ya nguvu ya viungo. Mexico na Madagaska hutoa vanila bora zaidi ulimwenguni.