Hasara za baada ya mavuno: Kukausha mpunga kwa kutumia kikaushio cha BAU-STR

0 / 5. 0

Chanzo:

https://sawbo-animations.org/773

Muda: 

00:03:26
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

SAWBO
Mpunga uliokaushwa vibaya hukabiliwa na ukungu na wadudu, na hivyo kusababisha hasara. Ukaushaji wa mpunga ni mgumu haswa wakati wa mvua na mawingu, kwa hivyo unahitaji kutumia kifaa cha kukausha.
Kutumia kikaushio cha BAU-STR kukauka mpunga hupunguza gharama za vibarua na hatari za kiafya. Kikaushio cha BAU-STR kinajumuisha kipulizia, pipa la ndani, pipa la nje, bomba la kupitisha hewa moto na jiko. Pipa la ndani na pipa la nje hukaa kwenye sakafu yoyote tambarare, kipulizia huwekwa kwenye pipa la ndani, jiko huwekwa kando ya pipa lingine na bomba la  kupitisha hewa moto huunganisha jiko na kipulizia.

Vyanzo vya moto na nishati za kuendesha kikaushio

Nafaka zinapaswa kuwekwa sawasawa katika nafasi tupu kati ya pipa la ndani, damani ya plastiki hutumika kufunika sehemu ya juu ili kuzuia hewa ya moto kuvuja nje. mkaa wa maganda ya mpunga hukatwa katika vipande vidogo vya urefu wa sentimeta 2.5 ambavyo hutumika kama chanzo cha moto jikoni, na umeme au jenereta hutumika kuendesha kipulizia. Kipulizia hufyonza hewa moto kutoka jikoni kupitia bomba la chuma na kupuliza hewa ndani ya pipa la ndani. Hii hukausha mpunga.
Joto linalopulizwa kwenye mpunga lisizidi nyuzi joto 43 kwa mupunga wa kutumika kama mbegu, na nyuzi 50 kwa mchele wa kuliwa. Ili kuwa mpunga bora,  acha kwa muda wa masaa 4 hadi 5 baada ya kukauka.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:36Ukaushaji wa mpunga vizuri huhibiti ukungu na wadudu lakini ukaushaji wa mpunga ni mgumu hasa nyakati za mvua na baridi hivyo kuhitaji kutumia kifaa cha kukaushia.
00:3700:57Kikaushio cha BAU-STR kinaweza kutumika hata katika siku za mvua. Pia hupunguza gharama, vibarua na hatari za kiafya.
00:5801:23Kikaushio cha BAU-STR kinajumuisha kipulizia, pipa la ndani, pipa la nje, bomba la kupitisha hewa moto na jiko.
01:2401:34Nafaka zinapaswa kuwekwa sawasawa katika nafasi tupu kati ya pipa la ndani, damani ya plastiki hutumika kufunika sehemu ya juu ili kuzuia hewa ya moto kuvuja nje.
01:3502:07 mkaa wa maganda ya mpunga hukatwa katika vipande vidogo vya urefu wa sentimeta 2.5 ambavyo hutumika kama chanzo cha moto jikoni
02:0802:19 Kipulizia hufyonza hewa moto kutoka jikoni kupitia bomba la chuma na kupuliza hewa ndani ya pipa la ndan
02:2002:50Joto linalopulizwa kwenye mpunga lisizidi nyuzi joto 43 kwa mupunga wa kutumika kama mbegu, na nyuzi 50 kwa mchele wa kuliwa
02:5103:26Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *