Ufugaji wa nguruwe una faida kubwa, hata hivyo nguruwe huathiriwa na hatari kadhaa ambazo huhitaji mbinu sahihi za usimamizi.
Inashauriwa kufuga idadi ya nguruwe ambayo inaweza kushughulikiwa kwa urahisi kulingana na fedha zilizopo pamoja, na kujifunza kuhusu ufugaji wa nguruwe mapema kwa kutembelea wafugaji wenye uzoefu.
Mbinu za usimamizi
Tambua wauzaji wa chakula wanaoaminika, na pia tolea nguruwe maji kwa ukuaji bora.
Safisha zizi la nguruwe mara kwa mara, geuza na kuongeza matandiko mapya ili kudhibiti magonjwa.
Andika na uhakikishe utunzaji wa kumbukumbu ili kubainisha mapato na gharama za mradia kwa urahisi
Andika kiwango cha wastani cha chakula kinachotumika, na tafuta vyanzo vya maji nafuu ili kupunguza gharama za usimamizi.
Fuata ratiba za chanjo ili kudhibiti magonjwa.
Andaa mpango wa biashara ili uwe mwongozo wa ufugaji wa nguruwe, na chunguza gharama na mapato ya mradi ili kuandaa taarifa ya mapato.
Mwishowe hakikisha mbinu bora za usimamizi wa nguruwe ili kuongeza mapato na kudhibiti wanyama kufa.