Unaposhughulikia vifaranga, kuwachanja ni muhimu katika udhibiti wa magonjwa hasa ya virusi. Kujua wakati sahihi wa kuchanja ndege ni muhimu sana.
Kabla ya kupokea vifaranga wa siku moja, hakikisha kwamba chumba cha kuwatunzia kimetengenezwa vizuri, na kina chanzo cha joto, taa na matandiko. Unapopokea vifaranga, waondoe kwenye masanduku na uwaweke kwenye chumba cha kuwatunzia, na uwaache wapumzike kwa dakika 5. Baada ya dakika 5, wape maji safi yaliyochanganywa na chakula cha vifaranga kwa siku 3 za kwanza. Chakula cha vifaranga kina vitamini nyingi ambazo humsaidia kifaranga kustahimili mafadhaiko, na pia kina glukosi ambayo ni chanzo cha nishati.
Ratiba ya kuchanja
Katika siku ya 14, chanja vifaranga dhidi ya kideri na ugonjwa wa mapafu. Baada ya kuchanja, hakikisha kuwa huwapi ndege viuavijasumu vyovyote kwa sababu baada ya chanjo, kinga ya ndege huathirika.
Chanja ndege dhidi ya ugonjwa wa gumboro katika siku ya 20, kideri kwa siku ya 28 na pia gumboro tena katika siku ya 33.
Chanja ndege dhidi ya ugonjwa wa tetekuwanga katika siku ya 42.
Katika siku ya 50, chanjo ndege dhidi ya kideri tena na hii ndiyo chanjo ya mwisho ya kideri. Wafugaji pia wanaweza kutumia chanjo ya LaSota ambayo hutolewa kwa ndege kwa njia ya kudunga sindano ndani ya misuli au chini ya ngozi ili kudhibiti kideri kwa muda wa kati ya miezi 6 hadi mwaka 1.