Ulaji wa mayai miongoni mwa ndege hupunguza mapato kwa wafugaji, na kadri ndege wanavyozidi kula mayai yao ndivyo inavyokuwa ngumu kutatua changamoto hiyo.
Sababu na suluhisho
Msongamano wa juu, hii ndiyo sababu kuu ya ulaji wa yai na inaweza kutatuliwa kwa kutoa nafasi ya kutosha kwa ndege au kuruhusu ndege kuwa huru. Nafasi iliyopendekezwa inapaswa kuwa futi 4 za mraba kwa kila ndege.
Kutokuwa na uwezo wa kutoa masanduku ya kutagia; Toa kisanduku 1 cha kutagia mayai kwa kila kuku 4 au tumia masanduku maalum ambayo huondoa mayai mara tu yanapotagwa.
Ukosefu wa maji; hii husababisha kiu na kwa hivyo toalea ndege maji safi ya kutosha.
Njaa; Toalea ndege malisho bora ya kutosha kila siku.
Lishe lisilosawazishwa; Ongeza kiwango cha protini na kalsiamu kwenye malisho.
Uchovu; wafanye ndege kufanya mazoezi au kuwaacha huru.
Mwanga mwingi katika banda la kuku; punguza mwanga katika masanduku ya kutagia.
Mfadhaiko; tumia mbinu huria wa ufugaji, au punguza msongamano wa kuku.
Kuku wasio na uzoefu pia hula mayai yao, kwa hivyo ongeza kiwango cha protini na kalsiamu katika malisho yao.
Udadisi; kusanya mayai mara tu baada ya kutagwa au fanya mbinu ya ufugaji huria.