»Jinsi ya kuanzisha biashara yako ya ufugaji wa nguruwe«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=E353Ipy4RCo&t=14s

Muda: 

00:15:02
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Best Farming Tips

Biashara ya ufugaji wa nguruwe huleta mapato ya haraka kwa vile dume hukomaa katika miezi 18, na jike ana muda wa ujauzito usiozidi siku 115. Nyama ya nguruwe huliwa sana.

Nguruwe huhitaji utunzaji na usimamizi bora. Mambo muhimu ya kuzingatia katika ufugaji wa nguruwe ni pamoja na ardhi, mtaji, na soko. Kuna njia mbili za ufugaji wa nguruwe, na hizi ni; mbinu ya banda na mbinu huria. Samadi ya nguruwe ni mbolea bora kwa wakulima na pia hutoa malisho kwa samaki.

Hatua za kuanzisha ufugaji wa nguruwe

Anza kwa kuchagua mbinu ya ufugaji wa nguruwe,eneo pa kuwafugia, idadi ya nguruwe wa kufugwa na lengo la soko. Fanya utafiti wa soko, uchanganuzi wa faida na gharama, na kisha andika mpango wa biashara.

Jenga banda ili kutoa kivuli kwa kuwa halijoto husababisha changamoto kubwa kwa wafugaji wa nguruwe

Hakikisha kwamba kuna hatua za kuzuia uenezaji wa magonjwa kutoka kwa mazingira ya nje. Lisha nguruwe chakula chenye lishe kilichochachushwa kwa siku 3.

Hakikisha unachachusha chakula cha nguruwe kwa vile kina afya zaidi kuliko chakula kikavu.

Hakikisha kuna kuna vifaa vya kupoesha na kuburudisha halijoto kwa kuwa nguruwe hawana tezi za jasho. Ondoa samadi ipasavyo ili kudhibiti magonjwa.

Hakikisha kuna makazi yanayofaa na uingizaji mzuri wa hewa ili kudhibiti hali mbaya ya hewa. Ruhusu nguruwe kulisha kwenye malisho ya majani.

Pia epuka kuchanganya nguruwe wa umri tofauti ili kupunguza kupigana.

Hatimaye, wasiliana na daktari wa mifugo iwapo kuna dalili za ugonjwa ili kutoa dawa haraka.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:33Nyama ya nguruwe huliwa na watu wengi sana. Na ufugaji wawo ni chanzo cha kipato
01:3402:06Nguruwe huhitaji utunzaji na usimamizi bora, na huleta kipato cha haraka.
02:0703:14Chagua mbinu bora ya ufugaji wa nguruwe, mahali pa kuwafugia, idadi ya nguruwe na lengo la soko.
03:1503:33Fanya utafiti wa soko, uchanganuzi wa faida na gharama, na kisha andika mpango wa biashara.
03:3405:01Jenga banda, na hakikisha kwamba kuna hatua za kuzuia uenezaji wa magonjwa.
05:0205:27Lisha nguruwe chakula chenye madini.
05:2806:08Chachusha chakula cha nguruwe. Hakikisha kuna kuna vifaa vya kupoesha na kuburudisha halijoto.
06:0907:03Ondoa samadi ipasavyo ili kudhibiti magonjwa.
07:0408:04Epuka kuchanganya nguruwe wa umri tofauti.
08:0508:40Tumia aina ya kienyeji ya nguruwe.
08:4109:59Mbinu za ufugaji wa nguruwe
10:0011:30Jenga banda bora lililo na mfumo mzuri wa uingizaji wa hewa, na ulishe nguruwe chakula chenye lishe kilichochachushwa kwa siku 3.
11:3112:06Viungo vya chakula cha nguruwe ni nafaka zilizochanganywa na protini, na madini.
12:0712:26Lisha nguruwe kulingana na umri na uzito wao.
12:2715:02Wape wanyama maji safi. Hifadhi dume 1 kwa kila majike 20, na wasiliana na daktari wa mifugo ikiwa kuna dalili za ugonjwa.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *