Kuanzisha ufugaji wa kuku ni rahisi lakini kuendeleza mradi huo kunahitaji pesa nyingi ili kununua chakula. Hata hivyo, kuna njia mbalimbali ambazo zimetengenezwa ili kufanya ulishaji wa kuku kuwa nafuu.
Mabuu ni chakula kizuri kwa ndege. Mabuu wanaweza kupatikana kwa urahisi na haraka kwa kuweka kinyesi cha sungura kwenye chombo kilichofungwa kwa siku 4. Vyakula vya nafaka pia vina manufaa makubwa kwa kuku miongoni mwa haya yanaweza kujumuisha soya, mtama na mahindi. Hata hivyo, haya lazima yasagwe ili kurahisisha umeng’enyaji.
Mbinu za kutumia
Lisha kuku kwa mabaki ya jikoni kwani haya ni chanzo kikubwa cha wanga na protini.
Kuku pia wanaweza kulishwa kwa mboga za majani pia kwani hizi hutoa vitamini na kalsiamu kwa ndege.
Pia lisha kuku kwa magugu na mabaki ya shamba kwani haya yana virutubisho vingi. Lisha ndege matunda kama vile zabibu, mapera, maembe kwa ajili ya kutoa vitamini C.
Hakikisha unawapa ndege mabuu, mchanganyiko wa nafaka zilizosagwa na mbegu za alizeti na pia tumia vyakula vya kuku vilivyochanganywa vizuri na mahindi yaliyosagwa.
Tumia nafaka ambacho zimechachushwa kwa siku 3, haya yana manufaa kadhaa kwa kuku na wafugaji kwani yanaweza kulisha idadi kubwa ya kuku.
Nunua chakula kwa wingi ili kufaidika punguzo kutoka kwa wauzaji.
Ruhusu kuku kujilisha huria ili wajitafutie chakula chao wenyewe, hata kuku hawa wanapaswa kuongezwa chakula kwa matokeo bora.