Kutengeneza mbolea oza husaidia kuongeza rutuba ya udongo kwa njia mbayo hutunza mazingira. Mbolea kawaida huwa tayari baada ya wiki 9.
Kuna faida kadhaa zinazohusiana na mbolea oza kama vile; ni rahisi kutengeneza kwani vifaa vinavyotumika ni rahisi kupatikana, mbolea oza haiathiri mazingira, hutengenezwa kwa bei nafuu, na haina athari kwa afya ya watu. Majani ya kijani hutumiwa katika mchakato kwa sababu yanaoza haraka.
Mchakato wa kutengeneza mbolea oza
Kwanza chagua eneo la mita 2 za mraba na chimba shimo la sentimita 30 huku ukiweka udongo wa juu kando.
Kisha tandaza mabua kwenye shimo na kisha ongeza majani makavu au mabichi yenye unene wa sentimita 15.
Kisha ongeza samadi ya wanyama yenye unene wa sentimita 10, ongeza udongo wa juu na kisha ongeza safu nyingine ya majani yenye unene wa 15cm.
Nyunyiza majivu juu, ongeza maji ili majivu yachanganyike na majani na udongo. Rudia utaratibu hadi rundo lifikie urefu wa mita 2.
Funika eneo lote na majani makavu na utandaze udongo juu ili kuzuia majani kupeperusha na upepo.
Ni muhimu sana kuchomeka kijiti katikati ya rundo ili kusaidia kuangalia halijoto la mbolea ili kuamua kwa urahisi kama mbolea iko tayari.
Jenga upya rundo la mbolea mara kila baada ya wiki 3 kwa kuchimba shimo jipya kando ya rundo na kuhamisha nyenzo huku ukitandaza safu ya juu kwanza ili kuharakisha mchakato wa kuoza.