»Sifa za dume bora«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=yb_41-pcMBk&t=78s

Muda: 

00:10:46
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Hamiisi Semanda

Dume ni muhimu katika kuzaliana. Kwa hivyo apaswa kuchaguliwa kwa uangalifu.

Dume huthaminiwa zaidi kuliko jike kwa sababu anaweza kuhamisha sifa zake bora kwa mifugo mingine. Kwa mfano, dume mmoja anaweza kuhudumia hadi majike 50 katika kipindi cha miezi 3 ya kuzaliana. Unapochagua dume kwa ajili ya kuzaliana, lazima awe na sifa bora, laa sivyo anaweza kueneza sifa duni katika kundi lako.

Aina safi/ chotara.

Dume kuwa na rangi nyeupe haimaanishi kwamba ni chotara au safi. Wanyama wa kienyeji wana uwezo wa kuwa na rangi yoyote.

Aina chotara hupendwa sana kwa sababu hukua haraka. Kupandishana aina safi na ya kienyeji huhamisha sifa bora ya utumiaji mzuri wa malisho kwa watoto. Aina za kienyeji huchukua muda mrefu zaidi kufikia 70kg na hicho ndicho kiwango cha juu wanachoweza kufikia, huku aina safi huchukua muda mfupi kufikia 70kg na wanaweza kufikia hadi kilo 120.

Aina safi zina pua za kirumi (pua zenye ncha kali) na pembe zao huunda nusu duara na uso. Masikio yao ni makubwa na marefu zaidi kupita midomo.

Madume kwa ajili ya kuzaliana

Dume kuwa mkubwa haimfanyi kuwa anafaa kutumika kwa kuzaliana. Mapumbu ya dume mzuri lazima yawe na ulinganifu na yasiwe marefu sana.

Madume wakuzaliana wanapaswa kuwa na mikia iliyosimama na wawe na rangi maalum. Hii husaidia kutambua aina yake.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:40Madume huthaminiwa zaidi kuliko majike katika kuzaliana
01:4103:04Dume mmoja anaweza kuhudumia hadi majike 50 katika kipindi cha miezi 3 ya kuzaliana.
03:0503:53Unapochagua dume kwa ajili ya kuzaliana, lazima awe na sifa bora.
03:5404:30Dume kuwa na rangi nyeupe haimaanishi kwamba ni chotara au safi.
04:3106:05Aina chotara hupendwa sana kwa sababu hukua haraka
06:0609:45Sifa za dume bora wa kuzaliana
09:4610:25Dume wa kuzaliana anapaswa kuwa wa rangi maalum.
10:2610:46Hitimisho

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *