Banda linaweza kujengwa chini au kuinuliwa.
Banda lililoinuliwa ni ghali zaidi kuliko banda la chini kutokana na kiasi kikubwa cha mbao zinazohitajika katika ujenzi. Iwapo mfugajo ana miti yake na bei ya soko ni nafuu, ni bora kuitumia kujenga banda la mbuzi kuliko kuiuza kwa bei nafuu.
Umuhimu wa kuinua banda la mbuzi
Unapojenga banda la mbuzi lililoinuliwa, kunapaswa kuwa na nafasi zilizoachwa kati ya mbao za kutengeneza sakafu ili kuruhusu kinyesi na mkojo kupita. Ni makosa kujenga banda lililoinuliwa bila kuacha nafasi hiyo.
Ukiwa na banda la mbuzi lililoinuliwa, hauhitaji kulisafisha kila siku. Pia ikiwa wafanyakazi wako si wazuri katika usafi, ni bora ujenge banda lililoinuliwa.
Mazingatio ya banda lililoinuliwa
Unapojenja banda, hakikisha kwamba mbuzi wana eneo la kufanyia mazoezi.
Banda la mbuzi linapaswa kuwa mita 1.5 kutoka chini na pande zote ziwe zimefungwa ili kuzuia mbuzi kuingia chini ya banda kwenye kinyesi na mkojo. Urefu wa mita 1.5 kutoka chini unatosha kuruhusu mtu kuingia chini na kusafisha banda.
Katika banda lililoinuliwa, unaweza pia kuligawanya ili kuwa na zizi la watoto na sehemu zingine katika chumba hicho hicho. Unaweza pia kuitengeneza ili mbuzi wa sehemu tofauti waweze kutumia eneo moja la kunyunyiziwa dawa bila kuchanganyika pamoja.