Zao la ufuta hulimwa na wakulima wengi katika maeneo kame kwa vile mmea hustahimili ukame. Ufuta umekithiri virutubisho vinavyohitajika kwa ukuaji wa wanyama.
Ufuta una mafuta 40–50%, protini 25%, vitamini na madini kwa hivyo una faida kubwa za kiafya. Mafuta yake hutumika katika tasnia ya dawa, kutayarisha mikate na vipodozi. Kwa mavuno mazuri, panda aina maalum katika msimu unaofaa. Jua kwamba kila aina ya ufuta ina kiasi chake cha mafuta, kwa hivyo inashauriwa kupanda aina zinazotoa mavuno mengi kwa hekta.
Mbinu bora za kilimo
Anza kwa kuchagua udongo tifutifu wa kichanga usio na maji mengi sana kwa vile udongo kama huo huhifadhi unyevu. Hata hivyo, ardhi iliyochaguliwa inapaswa kuwa tambarare kwa kuwa ufuta haustawi vyema kwenye ardhi iliyo sawa.
Panda ufuta mwishoni mwa msimu wa mvua kwa vile mmea hauhitaji maji mengi kustawi. Tayarisha shamba vizuri ili kuzuia magugu kuibuka mapema. Unapopanda ufuta pamoja na mazao mengine, acha nafasi ya 75cm.
Palilia mara kwa mara wiki 4 baada ya kupanda ili kupunguza ushindani wa virutubisho. Punguza idadi ya mimea ili kuhimiza msongamano wa mimea ufaao. Unapotawanya, changanya mbegu na mchanga mkavu ili kuhakikisha muachano wa kutosha kati ya mimea.
Panda kilo 4–5 za mbegu kwa hekta na weka mbolea ya urea na NPK ili kustawisha mimea. Dhibiti wadudu kwa kutumia dawa inayopendekezwa ili kuzuia upotevu wa mavuno kwani ufuta huathiriwa sana na wadudu.