Kutokana na ongezeko la mahitaji ya bidhaa za kilimo, mbinu mbalimbali za kutengeneza mbolea oza ya kutosha kwa ajili ya kilimo-hai zimebuniwa.
Mbolea ya minyoo ni maarufu sana kwa wakulima wa kikaboni. Kuna aina 2 za minyoo ambao ni pamoja na ule ambao huchimba chini kabisa kwenye udongo na mwingine ambao huishi juu ya udongo. Minyoo ambayo huishi juu ya udongo hula 10% ya udongo na 90% ya nyenzo za kikaboni. Huwa anakula kiwango sawa na uzito wa mwili wake.
Utumizi wa mbolea
Katika ekari moja, kuna kilo 30–40 ya minyoo. Mbolea ya minyoo ina vichocheo kadhaa, na hivyo huifanya kuwa mboji kamilifu. Minyoo pia hukua kutoka kwa mayai, na kutoa mboji. Weka tani 1 ya mboji kwenye vitalu vya mbegu ili kuboresha ukuaji na afya ya miche. Pia ongeza kilo 0.5 za mboji kwa kila mmea wakati wa kupanda na baada ya siku 45. Weka kilo 5–10 za mboji kila mwaka kwa miti mikubwa zaidi. Ongeza maji kwenye matangi ya minyoo na kisha uyakusanye kama mbolea minyoo ya maji. Hii ni mchanganyiko bora wa virutubishi, na vichocheo na hutumika kama kinga nzuri ya wadudu na magonjwa kwenye mazao.
Usindikaji wa mbolea
Minyoo wakubwa asili ya kiafrika hutumiwa. Hawa hustawi kwenye joto la 25–30 na unyevu wa 40–45%. Kisha majani makavu, mabaki ya mazao, makapi ya miwa nakadhalika huongezwa kwenye minyoo. Wakati wa kutekeleza mchakato, epuka kutumia maua ya glyceria na mmea wa tumbaku. Nyunyiza maji na changanya samadi ya ng‘ombe na nyenzo zitakazotumika, kisa weka mchangayiko chini ya kivuli kwa wiki 3–4. Hii kisha hulishwa kwa minyoo.
Jenga paa juu ya matangi ya mboji ya minyoo ili kuzuia mvua na jua ya moja kwa moja. Jenga matanki ukitumia mawe au saruji. Punguza ukubwa wa tanki na toboa tundu chini yalo ili kutiririsha maji ya ziada. Weka safu ya nyenzo zisizo laini chini ndani mwa tanki, na safu ya nyenzo za kikaboni na samadi mbichi ya ng‘ombe juu yake.
Weka safu nyingine ya nyenzo za kikaboni na urudie kutekeleza uratatibu huo hadi tanki litakapojaa. Eneza minyoo juu na umwagilie maji ili kudumisha unyevu. Mbolea huwa tayari baada ya miezi 2–3 kulingana na nyenzo zilizotumika. Kusanya mbolea ya minyoo kutoka juu, na uichuje baada ya kuondoa unyevu wa ziada. Endelea na utayarishaji wa mbolea hii kwa kuongeza nyenzo nyingine kwenye tanki. Jenga sakafu la saruji katika eneo la kutengenezea mboji ya minyoo. Weka mifereji ya maji au majivu karibu na tanki la minyoo ili kudhibiti mchwa. Epuka kutumia viuatilifu.