Mboji ya mbolea huleta kipato kwa wakulima. Minyoo wa Kiafrika hukua hadi urefu wa inchi 5–6, wana uwezo wa juu wa kuzaliana, na pia huishi hadi miaka 2.5.
Hata hivyo, wakati wa mchakato huu, ongeza mboji ya minyoo iwapo minyoo hawapatikani ili kuwezesha mayai kuanguliwa. Ni muhimu kuweka saruji kwenye sakafu ili kudhibiti ndege, utitiri na panya kuingilia masanduku ya kutengenezea mboji ya minyoo, kwani wanaweza kuua minyoo. Zaidi ya hayo, jenga mfereji wa maji kuzunguka tanki, nyunyiza majivu ili kuzuia mchwa, usitumie viuatilifu na epuka mimea yenye harufu.
Hatua za kufuata
Chagua minyoo aina ya kiafrika kwa vile uwezo wao wa kuzaliana ni wa juu zaidi kuliko minyoo wa kisasa. Wotolee joto la kutosha kati ya nyuzi joto 25 – 30 Celsius, na unyevu wa asilimia 40 – 45%. Weka paa kwenye matangi ili kuzuia mvua na jua kuingia moja kwa moja kwenye mboji. Tangi linapaswa kujengwa kwa upana wa futi 3–4, kina cha futi 2–3 na urefu unaofaa.
Toboa tundu chini ya tangi ili kuondoa maji ya ziada na kukusanya mbolea ya minyoo ya maji. Weka safu ya nyenzo nzito chini mwa tangi, kisha ongeza safu ya nyenzo za kikaboni, pamoja na samadi ya mifugo na endelea kufanya utaratibu huo hadi tanki litakapojaa.
Weka hadi minyoo 25 juu ya nyenzo kwa kila futi ya mraba. Iwapo minyoo hawapatikani eneza mboji ya minyoo kwenye tanki kwa kuwa ina mayai ambayo yanaweza kuanguliwa.
Daima, nyunyiza maji juu ili kudumisha unyevu ndani ya matangi na hivyo kuhimiza maisha ya minyoo. Kusanya mboji ya juu, ikaushe ili kuondoa unyevu wa ziada, ichuje na kisha rudisha nyenzo kwenye tanki.