Kuna aina tofauti za dawa ya kuogesha mifugo zinazotumika katika udhibiti wa kupe lakini tahadhari zinapaswa kuchukuliwa wakati wa kutumia dawa hizo ili kuepuka kusababisha uharibifu kwa watu, wanyama au mazingira.
Kemikali zinazotumiwa zaidi zimeainishwa kama organophosphates, amidines, pyrethroids za viwandani na pyrethroids za asili. Organofosfati huua kasi lakini huwa na muda mfupi wa ulinzi wa siku 2 hadi 3. Amidines kama vile amitraz na triatix zina muda uliongezwa wa ulinzi kulingana na viwango vilivyotumika. Pyrethroidi za viwandani kama decatix zina ulinzi mrefu zaidi wa siku 7 hadi 10, na pia hudhibiti wanyama dhidi ya nzi wa mbung’o. Parethroidi asilia kama vile coopers pia zinaweza kutumika.
Kuvaa nguo za kinga
Dawa inayochaguliwa inategemea idadi ya vipengele, ambavyo ni pamoja na; vifaa vinavyopatikana, bei ya dawa na ufanisi dhidi ya vimelea vingine kama vile utitiri, chawa na nzi. Liche ya dawa inayotumika, nguo za kinga kama vile ovaroli na glavu zinapaswa kuvaliwa wakati wa kushughulikia kemikali kali. Wakati wa kushughulikia organophosphates, apron ya kuzuia maji pia inashauriwa. Bidha za kutumika tayari moja kwa moja zinafaa pia zitumike kama glavu za kinga zimevaliwa.
Barakoa lazima ivaliwe ili kuzuia kuvuta kemikali.
Ushauri juu ya matumizi ya kemikali
Ikiwa kemikali yoyote (iliyokolea au iliyoyeyuka) imagusana na mwili wako, ioshe mara moja. Vyombo vyote vya kemikali vinapaswa kuwekwa mbali na watoto, na kuharibiwa vikiwa tupu.
Wauzaji wa dawa za mifugo wanaweza kutoa ushauri kuhusu dawa bora zaidi kwa hali yako, na usaidizi wa huduma zozote mbalimbali.