Kupe ni moja ya changamoto kubwa katika uzalishaji wa mifugo. Kutumia majosho, bomba la mashine na kumwaga dawa ni baadhi ya njia za kawaida za kudhibiti kupe na magonjwa yanayoenezwa na kupe barani Afrika.
Wakati wa kuanzisha josho la kuogesha mifugo, uchaguzi wa eneo linalofaa ni muhimu sana. Eneo linapaswa kuwa tambarare, karibu na chanzo cha maji na shimo la kutupa chupa, na eneo hilo lazima lifungwe kwenye uzio. Mjao wa josho unapaswa kujulikana, na lazima kuwe na mahali pa kuoshea miguu mlangoni ili kua viini. Kunafaa kuwa na paa, pamoja na kuta nzuri ili kuepuka upotevu wa dawa. Njia ya kutoka kwenye josho inapaswa kuteremka ikielekea nyuma kwenye josho.
Hatua nyingine za udhibiti wa kupe
Kando na majosho ya kuogesha mifugo, hatua zingine za kudhibiti kupe ni pamoja na kunyunyiza dawa kwa kutumia bomba la mashine, bomba la mkono, na dawa za kumwaga.
Kunyunyizia kwa mikono kwa kutumia pampu ya ndoo ni nzuri kwa idadi ndogo ya mifugo, lakini tahadhari maalum zinapaswa kuchukuliwa kwa sehemu ambapo kuna kupe nyingi sana.
Kiwango kidogo cha dawa iliyokolea kinaweza kuwekwa kwenye sehemu mahususi ambapo kuna kupe nyingi sana, japo kuwa ufanisi waki ni mdogo.
Dawa za kumwaga za aina ya Pyrethroids za viwandani zinaweza kutumika zikiwekwa kwenye mstari wa kati kutoka kwa bega la ngombe hadi mkia, ama juu kwa kichwa kati ya masikio, na kwenye mkia. Mafuta yalio kwenye dawa za kuua wadudu huziwezesha kuenea polepole kwa mnyama wote, lakini ng‘ombe lazima awe kavu wakati wa kuweka dawa.
Udhibiti kwa mfumo wa majosho
Katika mbinu zote mbili majosho, dawa lazima ipimwe kwa usahihi ili kudumisha ukolezi sahihi. Ongeza dawa kwenye josho baada ya kila mara ya kuogesha ng’ombe au baada ya kila kuogesha ng‘ombe 500. Uongezaji wa dawa unaweza kufanywa kwa njia ya kawaida ambapo kiasi cha maji kinachohitajika kujaza kinakokotolewa kwa kutumia kijiti kilichopimwa na hivyo dawa inayohitajika kuongezwa. Ujazajia unaweza pia kufanywa kwa njia ya kuhesabu idadi ya ngombe ambapo huamua ni kiasi gani cha dawa kinachoitajika kuongezwa baada ya kuogesha idadi fulani ya wanyama kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Baadhi ya watu hutumia mkakati wa kujaza upya ambapo dawa mpya hutayarishwa kila wakati baada ya kuogesha ng’ombe.
Katika mkakati kutumia bomba la mashine, hakikisha kwamba tundu zinazopitisha dawa zinafanya vizuri, shinikizo ni sahihi na kuwe na eneo la kuoshea mguu kwenye mlango. Kiasi fulani cha dawa lazima kiongezwe baada ya kila ng‘ombe 100 kunyunyiziwa, kulingana na maagizo ya mtengenezaji.