Mikakati jumuishi katika usimamizi wa rutuba ya udongo hutegemea kwa nguzo nne ili kufanikiwa na mavuno.
mazao hayawezi kukua vyema udongo ukipoteza rutuba. Unaweza kuboresha udongo kwa kutumia mbolea ya kikaboni, mbolea ya madini, aina za mazao zilizoboreshwa, na mbinu nzuri za usimamizi wa ukulima, pamoja na kuzoeza mazao hali ya eneo lako. Utaratibu huu unaitwa „ Mikakati jumuishi katika usimamizi wa rutuba ya udongo“ na imegawanywa katika nguzo nne. Udongo hutofautiana na kwa hivyo humenyuka tofauti kwa mbolea za madini na za kikaboni. Udongo ambao humenyuka kwa mbolea huboresha mavuno ukipata mbolea ya kutosha iliyoboreshwa. Udongo duni huhitaji zaidi ya hapo.
Nguzo nne
Nguzo ya kwanza ni mbolea ya madini. Inatoa virutubisho lakini ni ghali kabisa. Wakulima wengine hutumia kipimo kidogo cha mbolea, kwa sababu hata kiasi kidogo husaidia kuboresha mavuno. Wanaongeza kiasi kidogo kwa kila shimo la kupandia, na hivi huokoa pesa. Kwa mpunga uliofurika, wakulima wanapaswa kuongeza nusu ya chembe ili kupanua mazao hadi tani moja.
Nguzo ya pili ni kutumia mbolea ya kikaboni kama mabaki ya mazao, samadi ya wanyama na mbolea. Haya yana virutubisho kidogo kuliko mbolea ya madini, lakini husaidia udongo kuwa unyevu na laini. Mbolea ya kikaboni huongeza aina nyingi za virutubisho vidogo, kwa hivyo mimea hunawiri. Pia Unaweza kuwaruhusu wanyama wako wabaki shamabani usiku ili waache samadi yao na mkojo huko. Wakulima wengine hufuga mbuzi ili wakusanye samadi yao ambayo hutumiwa kutayarisha mbolea. Utengenezaji wa mbolea husaidia udongo kushika vitutibisho.
Nguzo ya tatu ni kutumia aina zilizoboreshwa. Aina zenye afya husaidia kuvuna zaidi na kuzuia magonjwa tofauti. Ikiwa udongo umeboreshwa, utazalisha zaidi.
Nguzo ya mwisho ni kuzoeza mazao hali ya eneo lako. Wakulima huzalisha aina tofauti na wanapaswa kushughulikia mbinu nzuri ya usimamizi wa kilimo, ardhi na maji ili kujua ni ipi inaowafaa zaidi. Kwa ardhi yenye mteremko ni muhimu kuzingatia na kudhibiti mmomonyoko wa mchanga.