»Kudhibiti dumuzi wa mbegu ya embe«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/managing-mango-seed-weevil

Muda: 

00:12:08
Imetengenezwa ndani: 
2019

Imetayarishwa na: 

Biovision Africa Trust

Maembe ni matunda yaliyo na ladha nzuri lakini huathiriwa sana na wadudu kama vile dumuzi wa mbegu. Udhibiti wa mara kwa mara huboresha uzalishaji wa embe.

Dumuzi wa mbegu ya embe huharibu nyama na mbegu, na hivyo kusababisha matunda kuanguka mapema kabla ya kukomaa. Maisha ya dumuzi wa mbegu ya embe: Dumuzi waliyokomaa huwa kati ya rangi ya hudhurungi hadi kijivu kilichokolea. Rangi hii huwawezesha kuishi kwenye kokwa la mti wakati wa msimu wa matunda. Dumuzi hula maembe pekee, na wanaweza kuishi kwa muda mrefu bila kula. Dumuzi wazima huelekea kwenye matawi ili kuzaliana na kisha hutaga mayai ambayo huanguliwa na kuwa mabuu baada ya siku 3–4. Mabuu hupenyeza kwenye mbegu ambapo wataendelea kula mpaka wawe dumuzi wazima. Dumuzi wazima huacha mbegu na kuelekea na kujificha kwenye maganda ya mti, matawi au majani yaliyoanguka.

Mitego ya dumuzi

Daima, kuwa mwangalifu ili kutambua wadudu walioko kwenye bustani ya matunda, na kutumia utepe wenye gundi ambao hutega na kunasa dumuzi. Pia nyunyiza dawa za kuua wadudu. Hata hivyo, dawa hizi ni ghali na zina madhara kwa afya ya watu, mazingira na kuua wadudu marafiki shambani. Himizisha koyokoyo shambani ili waweze kula dumuzi. Choma mbangimwitu, pamoja na majani ya tithonia ili kutoa moshi ambao hufukuza dumuzi.

Zingatia mbinu bora za kilimo kama vile kuharibu matunda yaliyodondoka, kuzika matunda yaliyoanguka katika shimo la angalau 50cm ili kuua dumuzi wanaotokea. Mwishowe, kusanya na haribu matunda yaliyoanguka angalau mara moja kwa wiki. Pogoa miti ili kupunguza mazingira yenye unyevu ambayo hupendwa na dumuzi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:57Maembe ni matunda yanayopendwa na ni chanzo cha mapato.
00:5801:58Dumuzi huharibu nyama ya embe na mbegu.
01:5902:38Maisha ya dumuzi wa mbegu ya maembe. Dumuzi wazima huishi kwa koko la miti. hula maembe pekee, na wanaweza kuishi kwa muda mrefu bila kula.
02:3903:12Dumuzi wazima huelekea kwenye matawi ili kuzaliana na kisha hutaga mayai baada ya siku 3-4.
03:1303:33Baada ya mayai ya siku 3 – 5 mayai huanguliwa na kuwa mabuu.
03:3404:48Dumuzi wazima huacha mbegu na kutafuta maeneo ya kujificha. Huwa hawaruki.
04:4905:31Kudhibiti dumuzi wa mbegu ya embe. Kuwa mwangalifu na wadudu katika bustani ya matunda.
05:3207:00Tumia utepe wenye gundi. Nyunyizia dawa za wadudu
07:0108:03Himizisha koyokoyo shambani ili waweze kula dumuzi. Choma mbangimwitu, pamoja na majani ya tithonia.
08:0409:17Zingatia mbinu bora za kilimo kama vile kuharibu matunda yaliyodondoka
09:1809:41Zika matunda yaliyoanguka katika shimo la angalau 50cm
09:4210:13Kusanya matunda yaliyoanguka mara moja kwa wiki na upogoe miti.
10:1812:08Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *