»Kukausha pilipili kwa jua«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/solar-drying-chillies

Muda: 

00:11:35
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight

Pilipili isipokaushwa vizuri hupata unyevu, na ukungu huota na kutoa sumukuvu amabayo ni hatari kwa watu. Kikaushaji cha jua hutumia joto la jua kukausha pilipili.

Kukaushia kwa jua kuna faida kadhaa: pilipili hukauka kwa muda mfupi, hubakia na rangi yake nyekundu, huzuia ukungu, haiwezi kuingiza uchafu na vile vile hukausha vyakula aina mbalimbali.

Kutengeneza kikaushaji cha jua.

Vifaa: Mbao, misumari, bawaba, kufuli na damani ya plastiki.

Anza kwa kutengeneza fremu ya mbao kutegemea ukubwa wa bati. Paka bati rangi nyeusi ili kuvuta kiasi kingi cha joto la jua. Kisha tengeneza kikaushiaji kilicho na kina cha 30 cm. Urefu wote uwe wa 95cm kwa mbele na 110cm kwa nyuma.

Kwa bati la urefu wa mita 3, tumia jozi 3 za miguu ili kisimame vizuri. Upande wa juu wa kisanduku unainuliwa kidogo. Tengeneza mbinu ya kusaidia kutelezesha trei ikiwa 10cm juu ya sakafu ya kikaushiaji. Kwa upande wa nyuma, tengeneza milango 2 ya kusaidia kuweka na kuondoa trei kwa urahisi. Funika fremu za trei kwa nyavu ili hewa iweze kufikia chakula kutoka pande zote mbili. Telezesha trei ndani, ikiwa 10cm kutoka kwenye sakafu ili kukausha hewa inapitia na kukausha pilipili vizuri. Mwishowe funika upande mrefu kwa chandarua ili kuzuia vumbi na wadudu kuingia. Weka kufuli ndogo ya kufungia mlango.

Mchakato wa kukaushia kwa jua

Osha mikono ili kudumisha usafi wa bidhaa. Weka kikaushiaji kwenye eneo lililo na jua. Tandaza pilipili safi kwenye trei halafu uziweke kwenye kikaushiaji. Hakikisha umefunga milango kila wakati ili nzi wasiingie. Ikiwa kuna baridi usiku, weka kikaushiaji ndani ya nyumba ili kudhibiti ukungu

Baada ya kuanika kwa siku 2 angalia ikiwa pilipili zimekauka, kisha uzifungashe na kuzihifadhi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0002:14Kukausha pilipili sakafuni kunachukua muda. Kukausha kwa jua huharakisha mchakato.
02:1503:02Kikaushiaji cha jua hutumia joto la jua kutunza joto sawa.
03:0303:20Manufaa za kukausha kwa jua:
03:2105:11Pilipili hukauka kwa muda mfupi, hubakia na rangi yake nyekundu, huzuia ukungu, hakiwezi kuingiza uchafu na vile vile hukausha vyakula aina mbalimbali.
05:1205:18Kutengeneza kikaushiaji cha jua
05:1905:34Vifaa: Mbao, misumari, bawaba, kufuli na damani ya plastiki.
05:3505:55Tengeneza fremu ya mbao kutegemea ukubwa wa bati na Paka bati rangi nyeusi.
05:5606:09Tengeneza kikaushiaji kilicho na upanda wa mita 3. Urefu wote uwe wa 95cm kwa mbele na 110cm kwa nyuma.
06:0706:31Kwa bati la urefu wa mita 3, tumi jozi 3 za miguu, na upande wa juu wa kisanduku unainushwa kidogo.
06:3206:42Tengeneza mbinu ya kusaidia kutelezesha trei ikiwa 10cm juu ya sakafu ya kikaushiaji.
06:4307:26Kwa upande wa nyuma, tengeneza milango 2. Funika fremu za trei kwa nyavu. Teleza trei 10cm ndani ya kikaushiaji.
07:2708:20Funika upande mrefu kwa chandarua. Weka kufuli ndogo
08:2108:29Kukausha pilipili kwa jua
08:3008:58Osha mikono, weka kikaushiaji kwenye eneo lililo na jua. Tandaza pilipili safi kwenye trei halafu uziweke kwenye kikaushiaji.
08:5909:21Hakikisha umefunga milango wa kikaushiaji. Ikiwa kuna baridi usiku, weka kikaushiaji ndani ya nyumba
09:2209:47Baada ya siku 2 angalia ikiwa pilipili zimekauka, kisha uzifungashe na kuzihifadhi.
09:4811:35Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *