Kuunganisha miche kunajumuisha kuambatanisha seheme ya juu ya mmea, ambayo hugeuka kuwa matawi na majani, kwa sehemu ya chini iliyo na mizizi mzima, ambayo hukua kama msingi wa mmea. Miche iliyounganishwa hukomaa mapema na kutoa mavuno bora ya hali ya juu.
Pandikiza / unganisha miche kabla ya msimu wa mvua ili utomvi uweze kuambatanisha sehemu ya juua na sehemu ya mizizi. Safirisha sehemu hizo za mmea kwa uangalifu, ili kuepuka uharibifu. Maembe yana vitamini nyingi, na ni chanzo cha mapato.
Kupanda sehemu ya mizizi
Chagua matunda ambayo hayajaharibiwa na uyatoe maganda. Jaza mifuko midogo na udongo wenye rutuba (mboji) kwa ukuaji mzuri wa mbegu. Weka mbegu kama upande ulioelekezwa ukiangalia juu ili kuota vizuri. Weka mifuko kwenye mahali pazuri na umwagilie maji kwa ukuaji bora. Baada ya kuota, chagua miche yenye afya tu na uweka mifuko kwenye udongo ukiacha nafasi ya kutosha kwa uunganishaji rahisi.
Utaratibu wa kuunganisha
Chagua sehemu ya juu na sehemu ya mizizi zilizo na sifa zinazohitajika kama vile kuwa sugu dhidi ya magonjwa, kutoa bidhaa sana, kuwa na kipindi kifupi cha ukuaji, na chipukikizi laini. Kata shina linalofaa la urefu wa 20cm. Kata sehemu ya juu ya urefu wa 10cm kutoka kwa shina hilo.
Kwa uunganishaji wa kabari, ambatanisha sehemu ya juu na sehemu ya mizizi iliyo na miezi 8, na kisha uzifunge na plastiki nyembamba. Kwa uunganishaji wa upande, sehemu ya mizizi ya mwaka 1 hukatwa ikiteleza/ ikipinda na kuwekwa kwenye seheme ya juu ya mche na kuziunga na plastiki nyembamba. Unaweza pia kukata matawi madogo ili kupunguza utumiaji wa virutubisho. Mara majani yanapogeuka kijani, hapo basi mimea iko tayari kuuzwa.