Maharagwe ya kutambaa hutoa mavuno mara tatu zaidi ya maharagwe ya msitu, na ni tamu kuliko maharagwe haya. Walakini, ndege panya (puaju) huharibu sana mavuno.
Ndege panya/ puaju ni wembamba, rangu ya hudhurungi au kijivu, na urefu wa sentimita 10. Wana mkia mwembamba mara mbili urefu wa mwili wao. Puaju hula mimea, mashina machanga, majani machanga, maua, maganda machanga, matunda na mbegu. Ndege panya huvamia shamba katika vikundi vya ndege kama 30, na wanaweza kuharibu shamba mzima. Wanajificha kwenye miti iliyo karibu, na mashamba ya ndizi. Uharibifu ni ukubwa sana wakati mimea hutoa maua.
Vifaa vya kutisha ndege
Weka kifaa chochote cha kutisha kabla ya maua kufunguka, na ubadilishe vifaa hivyo vya kutisha mara kwa mara. Unaweza pia kuwatisha ndege kwa kutoa sauti shambani asubuhi na mapema. Ikiwa wakulima wanapanda katika kipindi hicho hicho, ndege watafanya uharibifu mdogo kwa mavuno. Kuwa na ndizi, na mimea tofauti iliyo na maua na matunda karibu na shamba la maharagwe husaidia kuwaelekeza ndege mbali na maharagwe.