Kubadilisha malkia mzee na malkia mchanga kwenye mzinga ni muhimu katika kuongeza tija ya mzinga wa nyuki.
Hili hufanywa kila mwaka na wafugaji wa nyuki wa kibiashara ili kupata manufaa kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa kemikali maalum, na uwezo wa malkia wachanga kutaga mayai. Wafugaji wa nyuki kitafrija wana uwezekano mkubwa wa kubadilisha malkia kila baada ya miaka 2. Wakati wa kubadilisha malkia, malkia mzee anapaswa kutafutwa na kuuawa au kutupwa mbali. Malkia wa nyuki wenye afya na ambao wametunzwa vyema na wenye maumbile bora, pamoja na masega mazuri ya nyuki kibarua ni sababu kuu katika kuongeza mavuno ya asali.
Mchakato wa kubadilisha malkia
Kubadilisha malkia ni bora kufanyika wakati nyuki hawaruki aau kuhama, na ambapo kuna nekta na chavua vingi. Ikiwa unabadilisha malkia wakati nyuki wanaruka, kuna uwezekano wa kumpoteza malkia mpya pamoja na kundi la nyuki.
Iwapo unanunua malkia, malkia waliojamiana huwekwa katika vizimba vya miundo tofauti pamoja na nyuki 4 au 5 wa kuwasindikiza.
Chagua malkia ambao watoto wao ni wataweza kuzaa, sugu kwa magonjwa na watulivu. Kizimba ambacho kimetiwa malkia mpya na msindikizaji huwekwa kati ya masega 2 katikati ya kiota. Angalia baada ya siku 10 ili kuhakikisha kama malkia mpya amekubaliwa katika kundi la nyuki.
Unapobadilisha malkia, inashauriwa kuondoa malkia mzee kutoka kwenye mzinga siku iliyopita, na kuweka ndani seli za malkia siku moja kabla ya kuangua.
Kama ilivyo kwa mbinu nyingi za usimamizi, ni muhimu kudumisha usafi na usalama ndani ya mzinga wakati wa kubadilisha malkia.
Wiki sita hadi nane baada ya kubadilisha malkia, nyuki vibarua wote watabadilika yaani inawezekana kuanzisha hisa bora ya maumbile kwa muda mfupi.