Kanuni za usimamizi wa mwavuli wa miparachichi

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=OiA8v3W9gI8

Muda: 

00:07:36
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Queensland Agriculture
Usimamizi sahihi wa mwavuli wa miparachichi huruhusu jua kupenya vizuri kwenye miti, hivyo kuwezesha ukuzaji wa matunda pamoja na kuwezesha usimamizi bora wa miti, jambo ambalo huongeza mavuno.
Katika usimamizi mzuri wa mwavuli punguza matawi ya mti ili uweze kuwa saizi kidogo na hivyo kupunguza pembejeo zinazohitajika na mti kustawi. Waweza kufungua mwavuli ili kuruhusu mwanga wa jua kupenya. Miti midogo na mifupi huzaa matunda mengi zaidi. Usimamizi wa bora wa mwavuli hupunguza gharama za kupogoa miti

Usimamizi sahihi

Panga mradi wako wa usimamizi wa mwavuli mapema, na katika mashamba yenye msongamano mkubwa wa mimea hakikisha utunzaji wa mwavuli wa mara kwa mara. Pia hifadhi matawi ya chini iwapo shamba linakabiliwa na joto, baridi na ukame ili kuunda mazingira ambayo yanaweza kulinda mti. Pogoa miti mara kwa mara katika mazingira ya joto. Wakati wa kupogoa hakikisha kwamba urefu wa mti hauzidi 80% ya urefu wa mimea iliyopandwa kati ya safu, na hivyo unapaswa kuwa urefu wa 5m ili kurahisisha usimamizi.

Shughuli zilizowekwa

Daima punguza ukubwa wa mwavuli usiozaa matunda, na hakikisha kuwa matawi yametenganishwa. Pia kupogoa kunapaswa kufanywa wakati wa miezi ya baridi ili kuzuia kuota tena kwa mimea. Zuia jua la moja kwa moja ambalo huchoma matunda machanga na matawi mapya. Mwishowe, pogoa matawi mara baada ya kuvuna hii kusaidia miti kujenga akiba ya wanga, na pia kupunguza ushindani wa virutubisho.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:38Usimamizi mzuri wa mwavuli wa miparachichi husababisha mavuno mengi.
00:3901:36Katika usimamizi mzuri wa mwavuli punguza matawi ya mti ili uweze kuwa saizi kidogo ama aweza kufungua mwavuli
01:3702:10Panga mradi wako wa usimamizi wa mwavuli mapema
02:1102:33hifadhi matawi ya chini iwapo shamba linakabiliwa na joto, baridi na ukame ili kuunda mazingira ambayo yanaweza kulinda mti
02:3403:24 Hakikisha kwamba urefu wa mti hauzidi 80% ya urefu wa mimea iliyopandwa kati ya safu, na hivyo unapaswa kuwa urefu wa 5m ili kurahisisha usimamizi.
03:2504:06Punguza ukubwa wa mwavuli usiozaa matunda
04:0705:04Anza usimamizi wa mwavuli mapema na pogoa wakati wa miezi ya baridi.
05:0506:08pogoa matawi mara baada ya kuvuna hii kupunguza ushindani wa virutubisho.
06:0907:36Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *