Jinsi ya kuvuna asali

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=xnhmxNoo4EY&t=16s

Muda: 

00:08:47
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Maddie Moate
Asali ni moja wapo ya bidhaa muhimu katika ufugaji wa nyuki, na uvunaji sahihi wa asali ni muhimu katika kudumisha ubora wa asali.
Kabla ya kuingia kwenye safari ya kwenda kuvuna asali, vaa vaazi la kujikinga dhidi ya kuumwa na nyuki. Lazima uwe na kitoa moshi, brashi laini ya kuondoa nyuki kwenye masega, na kifaa cha kufungulia mzinga.

Uvunaji wa asali

Fungua mzinga wa nyuki na uangalie masega yaliyojazwa na asali. Acha masega yaliyojazwa nusu ili kuwawezesha nyuki kuyajaza asali kikamilifu. Baada ya kuondoa masega nje, funika tena mzinga.
Weka masega kwenye wilibaro (toroli) na uyafunike. Chukua masega kwenye chumba cha usindikaji ambapo asali huchimbwa kutoka kwenye masega na huchakatwa.
Ondoa safu ya juu ya nta kutoka kwa asali kwa kutumia kisu, na kisha weka masega yaliyo na asali kwenye zana ya kuchimba asali na uizungushe. Hii huondoa asali kutoka kwenye masega.
Baada ya kuzungusha, ruhusu asali kujikusanyia chini ya kifaa. Fungua bomba la kifaa ili kuruhusu asali kutiririka kupitia vichujio hadi kwenye ndoo. Kisha asali huwekwa kwenye chupa na kufungwa.
Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:25vaa vaazi la kujikinga dhidi ya nyuki
00:2601:29Vifaa vinavyohitajika wakati wa kuvuna asali.
01:3003:40Fungua mzinga wa nyuki na uangalie masega yaliyojazwa na asali.
03:4104:55Weka masega kwenye wilibaro (toroli) na uyafunike
04:5605:35Ondoa safu ya juu ya nta kutoka kwa asali kwa kutumia kisu
05:3607:00weka masega yaliyo na asali kwenye zana ya kuchimba asali na uizungushe.
07:0107:45Chuja asali kwa kutumia vichujio.
07:04608:38 Asali huwekwa kwenye chupa na kufungwa.
08:3908:47Hitimisho

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *