Azola ni mmea unaoelea na hukua haraka kwenye maji. Huelea kama fungu ndogo la kijani kibichi na ferni inaonekana kama malazi ya kijani juu ya maji.
Azola ni lishe bora kwa ng‘ombe, samaki, nguruwe, na kuku. Pia hutumiwa kama mbolea kwenye shamba na hurekebisha nitrojeni. Kilimo cha azola kinahitaji uwekezaji mdogo, kwa hivyo ni malisho mbadala ya gharama ya chini na mbolea nzuri ya bayo.
Maandalizi
Samadi ya ng‘ombe hutumiwa kurutubisha mbolea ya mmea wa azola na pia hutoa virutubishi kwa mifugo. Changanya samadi kilo 1.5 ya ng‘ombe kwenye ndoo kisha changanya kilo 5 ya mchanga usio na mwamba na ongeza gramu 150 ya fosfati .Baada ya kutandaza HDPE , jaza HDPE, maji na samadi ya ng‘ombe ,mchanga na fosfati kwenye dimbwi na kurudia kila mara kwa siku 30 ili kutoa virutubishi vya kutosha kukua kwa azola. Mwisho, hamisha kilo moja ya mbegu za azola kwenye dimbwi la HDPE.
Kuvuna
Azola huongezeka haraka kwenye kivuli. Ndani ya siku 7–10 hufunika bwawa lote. Mavuno ya mmea wa azola huvunwa kwa kutumia trei ya plastiki kuwa na mashimo ya kumwaga maji. Azola inaweza kuvunwa kila siku. Osha azola ili kuondoa harufu ya samadi ya ng‘ombe na mimea mingine. Changanya malisho ya kibiashara na azola katika uwiano wa 1: 1 kulisha mifugo .Baada ya wiki mbili unaweza kulisha mifugo bila malisho ya kujilimbikizia. Azola husaidia kuongeza uzalishaji wa maziwa na mfumo wa kinga ya ng‘ombe.