Magugu ni adui mkubwa wa wakulima kwa sababu hushindana na mazao ili kupata virutubishi na madini.
Magugu yanapaswa kutofautishwa na malisho shambani ili kuepuka kuathiri mifugo.
Gugu aina ya datura lina sumu ambayo huua wanyama linapoliwa. Desmodium ni mmea wa kudumu unaopanda, na una majani madogo na mizizi mirefu. Mmea huu una protini nyingi, lishe bora, na huongeza nitrojeni kwenye udongo, na hivyo kuongeza mavuno. Mmea wa desmodium una protini ya takriban asilimia 15–25 na fumuele uliokati ya 56–76 %, na unaweza kudumu kwa misimu 8–10 ikiwa utatunzwa vizuri.
Mbolea bora
Desmodium inaweza kurutubishwa na (NPK) mbolea ya Nitrojeni, fosforasi na Potasiamu. Unaweza kutumia aina ya mbolea ya 23–23 au 17–17–17, lakini kwa desmodium, mbolea ya nitrojeni haihitajiki. Matumizi ya samadi ya ng‘ombe wa maziwa husababisha upungufu wa fosforasi.
Desmodium kwa kawaida ni bora kwa mbuzi wa maziwa, ndama kwa sababu inasaidia kupunguza gharama za chakula cha mifugo.
Kuanzisha kilimo cha malisho
Malisho hupandwa kupitia njia mbili; kwa kutumia mbegu ambapo mbegu hizo huzikwa kwa kina cha mm 2 kwenye udongo, na kisha humwagiliwa maji ya kutosha. Njia nyingine ni kwa kutumia sehemu ya mmea uliostawi tayari shambani. Mmea hung’ongolewa na sehumu yake iluyo na mizizi huondolewa na kupandwa.
Unapopanda, acha umbali wa futi 1 kwa futi 1. Mmea wa desmodium ulio na virutubishi duni huwa na rangi ya manjano, kumaanisha una fosforasi kidogo, protini kidogo na nitrojeni kidogo.
Masharti bora
Desmodium huhitaji udongo bora ambao huhifadhi maji vizuri. Hizi ni udongo tifutifu, n.k. Mbegu kwa kawaida huchukua muda wa siku 75– 90 kukomaa lakini kwa vipandikizi vya kwanza, huchelewa hadi takribani siku 150 ili kuchanua maua na kutoa mbegu.
Aina za kawaida za desmodium ni aina ya kijani kibichi na doa nyekundu ya hudhurungi, aina ya jani la fedha ambyo ina shina na majani yaliyofunikwa kwa nywelenywele. Iwapo asilimia 30% ya desmodium imetoa maua, jua kwamba mimea iko tayari kukatwa. Kata mmea kwa urefu wa inchi nne juu ya udongo.